Ukosefu wa mahakama katika eneo lolote kama kata na wilaya inaweza kusababisha ucheleweshaji wa kesi nyingi kutolewa maamuzi,mkuu wa wilaya ya Gairo Mh.Siriel Mchembe amebainisha hali ilivyo wilayani humo.
“Wilaya ya Gairo tangu kufunguliwa kwake mwaka 2011 haijawahi kuwa na mahakama ya wilaya jambo hili lina kwamisha shughuli za kimahakama wilayani hapa” Amesema Mh.Seriel.
Aidha kutokana na vitendo vingi vinavyo tokea kwenye wilaya hiyo hususani mimba za utotoni watuhumiwa wanapo bainika wanapaswa kupelekwa mahakamani ili kwamba kesi hizo zitolewe huku mapema iwezekanavyo lakini kwa sababu hakuna mahakama,hivyo inalazimika kesi hizo kuhamishiwa wilaya ya kilosa na kama kesi nikubwa inapelekwa mahakama ya hakimu mkazi ya mkoa wa Morogoro.
Hata hivyo kunaongezeko la mimba za utotoni kwenye vituo vya zahanati na vutuo vya afya,jambo linalo ongeza maswali kwa wataalamu wa afya na viongozi wengine wa serikali,akarejelea ahadi ya Mh. Raisi wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kuhusu kujengwa kwa mahakama ya wilaya ya Gairo,hivyo mwaka huu ujenzi wa mahakama hiyo utaanza kwani eneo limekwisha patikana.
Katika hatua nyingine Mh.Mchembe na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo wame andaa dodoso ambalo linawahusu watoto wanaofika kwenye vituo vya afya wakiwa na umri mdogo kujibu baadhi ya maswali,huu ukiwa ni mpango maalumu wa kuwabaini wahusika wa ujauzito huo.
Mh.Mchembe akatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano wakutaja wahusika wanao fanya uhalifu kwa watoto wadogo haijalishi anasoma au hasomi ilimradi hajafikisha umri wa miaka kumi na name,akipata ujauzito nikosa kisheria.