Shirika la kazi duniani ILO Tanzania,limebainisha zao na mikoa inayo ongoza kwa utumikishwaji wa watoto walio chini ya miaka kumi na nane(18).
Dr.Greyson Nyadzi yeye ni afisa mradi wa kuwatoa watoto kwenye maeneo ya utumikishwaji mashambani , amesema zao linalo ongoza kwa kipindi hiki ni zao la tumbaku,wakulima wa zao hili wanatumisha sana watoto.
Aidha mikoa inayo ongoza kwa utumikishwaji Dr.Nyadzi ameitaja kuwa ni “Tabora,Katavi,Mara,Lindi na Mtwara kwani mikoa hii ndio inayo ongoza hata kwa mimba za utotoni”
Hata hivyo Nyadzi ameiomba jamii ya kitanzania kuwa na upendo,huruma,Hofu na kuacha kuwatumikisha watoto kwenye maeneo mbalimbali kama vile,Mashambani,Nyumbani,viwandani,Migodini hata kwenye maeneo ya Uvuvi,kwa kuendelea kufanya hivyo nikuwadumaza watoto na kuwanyima hakizao zamsingi kama watoto.