Hapa hospitali hakika wana jitahidi kutoa huduma kwa Mama na mtoto maana kabla hujajifungua unakuwa unapewa elimu ya namna ya kulea mtoto ikiwemo umuhimu wa kumnyonyesha mtoto kwa kipindi kinachotakiwa.
“Baada ya kujifungua tumewekwa kwenye darasa wanawake wote tuliojifungua tunafundishwa vyakula vinavyo takiwa kutumia wakati huu na ikiwemo na kuepuka hasira,kwani hasira husababisha kukosa maziwa ya kutosha wakati wakumnyonyesha mtoto”
Hayo ni maneno ya Christina Joseph mzazi alie jifungua katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa morogoro, wakati TKT/UN RADIO ilipo watembelea hosipitalini hapo kutaka kufahamu wanavyo elewa na kuzingatia wiki ya unyonyeshaji ambayo huazimishwa kila ifikapo 01-7, August ya kila mwaka.
Aidha Dr. Deborah Loganuza yeye ni Daktari mkuu wa kitengo cha Mama na mtoto hospitali ya rufaa ya mkoa wa Morogoro, amesema kilasiku wakina mama wanapo jifungua hupewa darasa jinsi ya kulea na umuhimu wa kuwanyonyesha watoto wao miezi sita ya mwanzo bilakuwalisha kitu au kuwanywesha chochote zaidi ya maziwa ya Mama.
Kaulimbiu mwaka huu inasema,”Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha watoto kwa afya bora na ulinzi wa mazingira”