“Tuwawezeshe wanawake kunyonyesha watoto kwa afya bora na ulinzi wa mazingira”
Hiyo ndio kaulimbiu ya mwaka huu katika wiki ya unyonyeshaji duniani ambapo hali inaonyesha kupiga hatua katika maeneo mengi nchini kwenye swala la unyonyeshaji maziwa ya Mama kwa zaidi ya asilimia tisini na tano 95 watoto wanao nyonyeshwa kwa mjibu wa takwimu za mwaka huu.
Nimezungumza na wanawake jamii ya kimasaai wanao Fanya biashara ya maziwa kutoka Dakawa Wilayani Mvomero,kuhusu wiki hii ya unyonyeshaji,wamesema kwa shalti la kutotaja majina yao harisi,
Royso Motonyi ameanza kwa kueleza”Sisi watoto wetu wakifikisha mwezi mmoja tu baada ya kuzaliwa tunaanza kuwanywesha maziwa ili wazoee, na kumlisha chakula kama uji na ugari ni baada ya miezi mitatu (3)-miezi minne(4) hatungoji hadi afikishe miezi sita(6) hasa tukiwa nje ya maeneo ya mjini yaani polini”
Bi, Motonyi amesema kwasasa jamii za kifugaji zinaendelea kuelimika kutokana na familia nyingi zina watoto walio soma na kuwa madaktari,walimu,bwana mifugo ,wauguzi nk, hivyo wana saidia kuelimisha familia zao kwa kushirikiana na serikali na wadau wa maendeleo vijijini.
Hata hivyo bi, Motonyi akatoa wito kwa serikali amesema “maadhimisho kama haya yanapaswa kufanyikia vijijini kwa jamii za kifugaji ili tuelimishwe vya kutosha kama vile muda wa kumnyonyesha mtoto maziwa ya mama kabla ya kumnywesha maziwa ya ng’ombe na chakula kingine“