Kwa mara ya kwanza katika historia ya shirika la kimataifa la kazi (ILO) kupitia mkataba wake wa kupinga ajira za utotoni wa kimataifa, umeridhiwa na nchi 187 zote wanachama ikiwemo Tanzania ,baada ya nchi ya Ufalme wa Tonga kutia saini kupitia kwa balozi wake Ndg.Titilupe Tuivakano iliokuwa imesalia kuukubali na kuutumia mkataba huo.
Akizungumzia hatua hiyo mkurungezi mkuu wa shirika la kimataifa la kazi (ILO) Ndug,Guy Ryder kupitia mkutano ulio fanyika August 4, 2020 Geneva Switzerland amesema kuthibitishwa kwa mkataba huo no.182 nihistoria inayomaanisha kuwa watoto wote sasa wanalindwa kisheria dhidi ya aina mbaya zaidi za ajira kwa watoto,kuridhia kwa nchi hiyo imefikia idadi ya nchi 187 wanachama wa shirika la kimataifa la kazi ILO zinazo pinga na kukomesha ajira za utotoni.
Aidha mkurungenzi huyo amebainisha kwamba “Ulimwengu umejitolea kupinga ajira za utotoni kama vile,Utumwa,Unyanyasaji wa kijinsia,Utumikishaji wa watoto vitani na katika kazi nyingine haramu au mbaya ambazo huleta athali kwa afya zao,Maadili au hali ya kisaikolojia kwa sasa hazina nafasi kwenye jamii yetu”.
Hata hivyo matarajio thabiti ya Kailash Satyarthi, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel,amesema “Ninandoto ya kuona ulimwengu umejaa watoto walio salama, Nina ndoto ya kuona ulimwengu ambao kila mtoto anafurahia uhuru wa kuwa mtoto” Mwisho wakunukuu.