Tangu kuanzishwa kwa ILO mnamo1919,kupinga ajira za utotoni limekuwa jambo la msingi kwa shirika hilo.Mkurugenzi wa kwanza wa ILO Albert Thomas alielezea ajira za utoto kwamba niza Unyonyaji kwa binadamu ambao husababisha ubaya na simanzi mioyoni mwao.
Matukio ya utumikishaji wa watoto na matukio mengine yalipunguwa karibu asilimia 40 kati ya mwaka 2000 na 2016,kama viwango kama viwango vya kuridhia na utekelezaji wa mkataba no.182 na mkataba no.138 kiwango kiliongezeka kwa nchi zilizo pitisha sheria na sera madhubuti kuhusu haki zinazo mlinda mtoto dhidi ya ajira za utotoni.
Aidha ripoti hiyo inasema pamoja na janga la Covid-19,kunahatari halisi kwamba mikakati ya maendeleo itabadilishwa na kusababisha ongezeko la ajira za utotoni kwa mara ya kwanza katika miaka 20 ingawa ripoti hiyo inazitaka nchi wanachama zichukue hatua zinazo faa dhidi ya utumikishwaji wa watoto.
Kukomesha ajira za utotoni ifikapo 2025 katika njia zote zilizo pendekezwa,nimoja ya njia zinazo ungamkono Lengo la 7.7 la Malengo ya Maendeleo Endelevu, yalio pitishwa na Mataifa yote ya jumuiya ya Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 2015.
Hata hivyo utafiti huo muhimu umekuja baada ya miezi michache kabla ya kuanza kwa mwaka wa kimataifa wa kutokomeza ajira za utotoni 2021,mpango huu unasimamiwa na ILO kwa kushirikiana na washirika,na kusudi lake kubwa ni kuongeza uelewa kwa jamii kuhusu vitendo vya utumikishwaji wa watoto ilikuhalakisha maendeleo.