Shirika lisilo la kiserikali la Save the Children kupitia mradi wake wa lishe endelevu lime wa wezesha zaidi ya waandishi wa habari 20 mkoa wa Morogoro kutoka kwenye vyombo mbalimbali vya Radio,Magazeti na Tv,kupewa mafunzo yakuandika na kuandaa vipindi vinavyo husiana na lishe ya mama na mtoto,lengo likiwa nikutoa elimu kwa jamii kuhusu namna ya kuzingatia unyonyeshaji kwa Mama na mtoto na kuondoa tatizo la utapia mlo katika mkoa huo.
Semina hiyo ilio fanyika katika ukumbi wa hospitali ya rufaa mkoa wa morogoro,ilio andaliwa na ofisi ya mganga mkuu kupitia kitengo cha lishe mkoa, Taasisi ya chakula na lishe Tanzania na kuwezeshwa na mashirika yasio ya kiserikali kama vile, Save the Children kupitia mradi wao wa lishe endelevu unao fadhiliwa na USAID.
Meneja miradi wa Save the Children mkoa wa Morogoro Ndg,Yahaya Nuhu amesema lengo kubwa la mradi wa lishe endelevu nikupambana na suala la udumavu na utapia mlo kwani kuna kiwango cha watoto zaidi ya laki moja 100,000 chini ya umri wa miaka mitano (5) wenye udumavu.
Kwaupande wake mganga mkuu mkoa wa Morogoro Dr.Kusirye Ukio amesema wameamua kutoa elimu kwa waandishi wa habari ilikwamba wawezekuandika na kuandaa vipindi vitakavyo endelea kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa lishe bora hasa kwa miezi 6 ya mwanzo mtoto anyonyeshwe maziwa ya mama tu pasipo kumpatia chakula au maji isipokuwa kwa maelekezo ya daktari.
Afisa lishe mkoa bi,Salome Magembe alitoa ufafanuzi na chimbuko la wiki ya unyonyeshaji duniani sababu zilizo sababisha kuanzishwa kwa wiki ya unyonyeshaji, miongoni mwa sababu ni Kabla na baada ya miaka ya 1980 dunia ilishuhudia tatizo la vifo vingi vya watoto wachanga na wadogo.
Aidha bi,Magembe amebainisha kuwa, Pamoja na juhudi za kuboresha huduma za afya, chanjo na matibabu ya magonjwa ya watoto bado hali ilibaki au kuzidi kuwa mbaya,Tafiti mbalimbali zilifanyika ili kubaini visababishi vya vifo vya watoto.
Hata hivyo bi,Magembe akaelezea hali ya lishe ya mkoa wa morogoro kuanzia 1992-2018 Morogoro inaonyesha kwamba watoto waliodumaa ni 106,730 ,ambayo sawa na 26.4%(watoto 26 kati 100), Watoto 14958 wana ukondefu sawa na asilimia 3.7%. Watoto 48917 sawa na 12.1% wana uzito pungufu.29.8% ya wanawake walio katika umri wa kuzaa wana upungufu mkubwa wa damu na asilimia 37.5% ya wanawake walio katika umri wa kuzaa wana uzito ulio zidi.