Maziwa ya ng’ombe yana protini isiyoweza kumeng’enywa kwenye tumbo la mtoto mwenye umri wa chini ya miezi 6 – Mtaalamu.
Ni mwaka mmoja tangu mradi wa mafunzo kuhusu lishe endelevu ulipoanzishwa mkoani Morogoro na shirika la Save the Children kwa ufadhili wa shirika la Marekani la msaada wa kimataifa USAID lishe endelevu.
Sehemu ya mradi huo ni kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa mtoto kunyonya maziwa halisi ya mama angalau kwa miezi sita ya kwanza bila kumpa chakula au kinywaji aina yeyote pamoja na kufundishwa uandaaji wa lishe bora.
AidhaMh. Mkuu wa wilaya ya mvomero Mh.Albinus Mugonya alie muakilisha mkuu wa mkoa wa morogoro Mh.Loata Sanare akaziagiza halmashauri zote kuhakikisha wana ungamkono wahudumu wa afya ya jamii walio pewa mafunzo maalum ya lishe,wanapo pita kutoa elimu ya lishe kwenye jamii.
Hata hivyo Mariam Mwita ambae ni mratibuwa mradi wa lishe endelevu,akasisitiza umuhimu wa kumyonyesha maziwa ya Mama halisi bila kumpa kituchochote kwa kipindi cha miezi 6 ya mwanzo,pia na kuzingatia muda wa kumuanzishia chakula mbadala.
Mradi huo unao tekelezwa na shirika la Save the children kwa ufadhili wa USAID lishe endelevu, unaolenga kuondoa udumavu,utapiamlo,uzito pungufu kwa watoto na upotevu wa damu kwa mama mjamzito ili kuboresha afya ya jamii.