Shirika la Save the Children kwa kushirikiana na serikali na mashirika mengine ya kijamii limeendelea kuelimisha jamii kuhusu mbinu za utokomezaji wa udumavu,utapiamlo na ukondefu kwa watoto chini ya umri wa miaka mitano na mama wajawazito.
Elimu hiyo inatolewa kwanjia yasemina kupitia kwa wa wakilishi kutoka kwenye vijiji ndani ya wilaya husika kwa ufadhili wa USAID Lishe endelevu,ambapo kila mmoja anapo hitimisha mafunzo hukabidhiwa vitendea kazi ikiwemo baiskeli.
Mkuu wa wilaya ya Mvomero Mh.Albinus Mugonya aka waasa wahudumu hao wa afya ya jamii walio pata mafunzo kabla ya kuhitimisha semina hiyo “tumieni elimu mlio ipata kuinufaisha jamii kwenye maeneo yenu kila mmoja aendako,muwe na heshima muingiapo kwenye nyumba za wananchi pasipo kukiuka miiko ya kazi yenu,serikali iko pamoja na ninyi kwenye mapambano haya ya kuboresha afya kwa njia ya lishe,hata Mimi kuanzia Leo ni balozi was lishe endelevu”.
Aidha bi,Joyce peter msimamizi mkuu wa semina hiyo kutoka shirika la Save the Children mkoa wa Morogoro, akaishukuru serikali kupitia mkuu wa wilaya ya Mvomero “Tunaishukuru serikali kupitia kwa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mvomero mh.Albinus Mugonya amekuwa balozi wa Lishe Endelevu kupitia mkoba wa siku elfmoja(1000) nakuitaka jamii kushirikiana na wataalamu walio pewa mafunzo hayo”.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki walioshiriki katika mafunzo hayo ya Sikh sita akasema atakapo fika kijijini kwao ataanza kuunda vikundi kama miongozo waliopewa kwenye semina ikiwemo kuzingatia umri kila kundi.
Hata hivyo bi,Feristar Malongo ambae ni mratibu wa mradi wa lishe endelevu kupitia shirika la umwema linalo tekeleza mradi huo kwa wilaya tatu ambazo ni Morogoro mjini,Morogoro Vijijini na Mvomero,akasema kiu yao kubwa nikuondoa tatizo la udumavu,ukondefu utapiamlo na lishe duni kwa mama wajawazito.