“Wamiliki wa vituo vya kulelea watoto nilazima visajiriwe msiendeshe vituo hivyo bila kusajili” Hayo yamejiri katika kikao kilichofanyika Ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Morogoro na kujumuisha Maafisa wa Ustawi wa Jamii, Mhandisi kalobelo amesema Tanzania inapojipanga kuelekea uchumi wa juu umuhimu wa Maafisa hao unazidi kutambulika na kwamba maafisa hao hawawezi kujiondoa kama sehemu ya kuipeleka nchi katika ustawi wa juu zaidi.
Kwaupande wao baadhi ya wadau wa masuala ya watoto amesema“Tunaona kweli watoto hawa ndani ya miayo yao wanaumia ”Hayo nimaneno ya Christina Wirner , mdau wa haki za watoto kutoka kituo cha kulelea watoto cha Agape kilichoko Kihonda mkoani Morogoro akieleza kuwa kutochukuliwa hatua kwa wale wanaonyanyasa watoto kunafanya matendo haya kushamiri katika jamii kiasi cha kuwafanya hata watoto wenyewe wageuke kuwa watu katili watakapokuwa wakubwa,“Tunahitaji kuwasaidia hawa watoto na pia naomba kwa serikali itusaidie” Amesema.
Aidha bi,Jesca Kagunila afisa ustawi wa jamii ngazi ya mkoa amesema kutokana namatukio yanayo jitokeza kwenye jamii , wadau wa masuala ya usalama wa mama na mtoto kamavile USAID Kizazi kipya mkoa wa Morogoro tayari wameunda kamati za kutokomeza ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Hata hivyo bi,Kagunila akatoa taarifa ya matukio ya mama na mtoto mkoa wa morogoro kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka huu jumla ya matukio 2848 ya ukatili yariripotiwa, kati yake matukio 1561 walifanyiwa watu wazima na matukio ya ukatili 1287 walifanyiwa watoto.
Katika matukio yote hayo ukatili wa kihisia umeonekana kuongoza kwa kuripotiwa matukio 1287 na kufuatiwa na ukatili wa kimwili matukio 699, ukatili wa kiuchumi matukio 551 na ukatili wa kingono matukio 111 huku Halmashauri ya Mji wa Ifakara ikiongoza kwa kuripoti matukio ya ukatili 1873,Katika matukio hayo yote matukio 157 ndio yalio fanyiawa kazi na matukio 19 tu, ndio yalio tolewa hukumu.
Akifunga kikao hicho kwa niaba ya Katibu Tawala wa Mkoa, ambaye baada ya kufungua alipata dharura, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt. Ukio Kusirye ametaka kuimarisha ushirikiano kwa wadau wanaofanya kazi za kuhudumia watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi na kuagiza ngazi za Wilaya nao kuitisha vikao kama hivyo.
Sophia Ngasso ni mkuu wa kitengo cha dawati la jinsia polisi mkoa wa Morogoro amesema juhudi zote hizo zinazochukuliwa ni za muhimu, lakini muhimu zaidi ni ushiriki wa jamii hususani wazazi katika malezi na ulinzi wa mtoto.