Jopo la madaktari bingwa kutoka katika tasisi isio ya kiserikali ya Same Qualities Foundation yenye makao makuu yake jijini Arusha kwa kushirikiana na serikali imeanza kutoa huduma zake za upasuaji kwa watoto wenye midomo sungura baada ya kuwa wamesitisha huduma hiyo kwa sababu ya virusi vya corona vilivyo ikumba dunia.
Huduma hiyo ilianza kufanyika mwezi June na August mwaka huu baada ya Corona katika mikoa ya Shinyanga na Kilimanjaro,upasuaji huo hufanyika bure kila kambi,na katika mkoa wa Shinyanga ulifanyika kwenye Hospitali ya Wilaya ya Kahama mkoani humo ambapo watoto 11 walifanikiwa kufanyiwa upasuaji.
Aidha mkurugenzi mtendaji wa tasisi hiyo Dr.Peter Mabula amesema kambi nyingine ya upasuaji ilio fanyika katika hospitali ya TPC Moshi mkoa wa Kilimanjaro mnamo mwezi Juni na Agosti mwaka huu, na watoto 20 walifanyiwa upasuaji.
Hata hivyo Dr.Mabula akatanabaish baada ya kufanya kambi ya upasuaji katika mikoa ya Shinyanga na Kilimanjaro kambi kama hiyo ikahamia mji mkuu wa Tanzania, Dodoma,ambapo huduma hiyo ilifanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kuanzia Agosti 23-28 na watoto 21 walifanikiwa kufanyiwa upasuaji kutoka kote nchini.