Jeshi la polisi mkoa wa Njombe limethibitisha kumkamata daktari wa hospitali ya Ikonda Dkt Mabula Pascal ambaye ni dereva wa gari lililowagonga watoto wawili wa kijiji cha Ng’anda hapo jana.
Aidha Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema chanzo cha tukio hilo ni ulevi wa pombe aliokuwa nao daktari wa hospitali ya Ikonda Wilayani Makete Mabula Pascal .
Hata hivyo katika tukio hilo lililotokea kijiji cha Ng’anda kata ya Makoga limesababisha kifo cha mwanafunzi anayesoma kidato cha kwanza katika shule ya sekondari Makoga Enieth Mligo na majeruhi Tukuzeni Mgeyekwa wa darasa la saba anaeendelea na matibabu kituo cha afya Makoga.
Katika hatua nyingine kamanda wa polisi mkoa wa njombe Hamis Issa amesema mtoto mwingine mwenye umri wa miaka minne amefariki kwa kugonjwa na gari aina ya canter mjini Makambako majira ya saa mbili usiku katika barabara kuu ya Iringa Mbeya.
Kamanda Issa pia amesema jeshi la polisi linamshikilia mzazi mmoja wa Matiganjora kwa tuhuma za kumuua mtoto Jesca Jairo mwenye umri wa miaka mitano aliyekutwa amefariki kando ya nyumba yao kwenye miti ya paina.