Wananchi Wilayani Njombe wametakiwa kuacha tabia ya Ukatili ikiwemo mauaji dhidi ya watoto ambayo yameendelea kujitokeza kwa baadhi ya maeneo Wilayani humo.
Rai hiyo imetolewa na mkuu wa Wilaya ya Njombe Bi Luth Msafiri akiwa katika kijiji cha Matiganjora kufuatia mama mmoja kutuhumiwa kumuua mtoto mwenye umri wa miaka 5 aliyekuwa anaishi nae.
Katibu tawala Wilaya ya Njombe Emmanuel Geoge ameshauri wananchi kutoa taarifa za matukio ya uharifu yanapotokea na kutaka kuacha tabia ya mauaji.
Msaidizi wa magereza Wilaya ya Njombe ASP Elioth Kingu amesema idadi kubwa ya wafungwa waliopo Njombe ni wafungwa wa mauaji ya watoto,huku Mkuu wa upelelezi Wilaya ya Njombe ASP Augustino Ndamgoba akisema mauaji mengi yanafanyika baina ya ndugu wenyewe.
Msemaji wa familia ya Jairo Mkanga Bwana Keneth Nyagawa akaeleza namna tukio lilivyotokea hadi mama wa kufikia kumfanyia ukatili wa mauaji mtoto wa mme wake kwa kumnyonga na kamba shingoni.
Nao wananchi wa kijiji cha Matiganjora wakiongozwa na mwenyekiti Bi. Grace Nyagawa wanaungana na serikali kukemea vikali tabia za mauaji ya watoto na kutaka serikali kuchukua hatua kali dhidi ya matukio wakiwemo wauwaji.
Hivi karibuni jeshi la polisi limemshikilia mama mmoja wa kijiji cha Matiganjora kata ya Ikuna Wilayani Njombe kwa tuhuma za mauaji ya mtoto.
Na,Michael Ngilangwa.