Wadau wa Elimu na waombwa kuendelea kuwasaidiwa wanafunzi wenye uhitaji maalumu mashuleni.
Hayo yamesemwa na Katibu tawala Wilaya ya KILOSA, YOHANA KASITILA katika zoezi la kuwapatia mahitaji wanafunzi wenye uhitaji maalumu katika Shule ya Sekondari ya Morogoro.
Miongoni mwa walioambatana na Katibu tawala huyo ni mwenyekiti wa kikundi cha MOSESCO ambacho ni muunganiko wa wanafunzi waliosoma mwaka wa 1989 mpaka 1992, ATHUMANI KAKIMA na CHERI IKANGA walisema jambo hilo kwao ni muendelezo na kwamba huo ni mwanzo wa kuonesha mfano kwa wengine.
JOSEPHU KAPYUNKA, ambaye ni makamu mkuu wa Shule ya Sekondari Morogoro alisema mahitaji ya wanafunzi wenye uhitaji ni mkubwa katika Shule hiyo kutokana na kuwa na Idadi ya Zaidi ya wanafuzi mia moja walio katika mazingira magumu Zaidi.
JOSHUA JUMA NA ROZA MKUMBWA ni wanafunzi wenye uhitaji maalumu Kidato cha tano wakiwa ni miongoni mwa waliopokea zawadi walisema kufurahishwa kwa kupatiwa mahitaji ya kusomea na kuwaomba wadau wengine wa Elimu kujitokeza.
Umoja wa wanafuzi waliosoma Shule ya Sekondari Morogoro kuanzia mwaka wa 1989 1992 MOSESCO waliwapatia mahitaji mabalimbali wanafunzi ikiwemo Madaftari, Kalamu za wino na Penseli, Soksi, Taulo za kike, Rula, Vifutio, Kanga na Vitenge.
Na mwandishi Hamad Rashid.
Kwa kweli ni Jambo jema lakini yote tunamshkuru mwenyezi mungu kwa kutuwezesha kufanya hivi