Shirika la CAMFED nchini Tanzania ni moja ya mashirika yanayopambana kuhakikisha yanachangia katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu SDGs ambayo yamepangiwa kuwa yametimizwa yote 17.
Lengo namba 4 linazungumzia elimu bora na lengo namba 5 linazungumzia usawa wa kijinsia, yote hayo yakiwa yanalenga kutomwacha nyuma mtu yeyote katika maendeleo ya ulimwengu ifikapo mwaka 2030.
Mapema mwezi huu shirika hilo lili andaa hafla ya kutambua mchango wa wasichana na wanawake waliopitia katika mikono na mafunzo ya CAMFED miaka mitano iliyopita kupitia mpango wa Dunia yangu bora na sasa wanawake hao wanawasaidia wasichana wengine walioko katika mazingira magumu.
Hafla hiyo ili fanyika katika ukumbi wa mikutano Shule ya sekondari KILAKALA Manispaa ya Morogoro, ambapo jumla ya wawezeshaji elimu ya utambuzi kwa wasichana na wanawake 70 wakitunukiwa vyeti vya kutambua mchango wao kutoka shirikia la CAMFED linalosaidia mpango wa Elimu na uongozi kwao.
Mkurugenzi wa Shirika la CAMFED TANZANIA, LYIDIA WILBARD alisema wana namba kubwa katika kuwasaidia wasichana wanao toka katika mazingira magumu kiuchumi,malezi na hata kielimu, ambapo tangu mwaka 2005 hadi sasa jumla ya wasichana Laki sita themanini na tatu elfu mia nne therathini na tisa wamesaidiwa na shirika hilo, katika Shule 455.
Muwakilishi wa Serikali kutokaTAMISEMI ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Roata Sanare aliwapongeza CAMFED na kuahidi kuwaunga mkono katika majukumu yao kwa ushirikiano mkubwa utakaotolewa na Serikali ya Tanzania.
Wanufaika wa mradi wa Dunia yangu bora mpango unaoratibiwa na CAMFED walikili kufaidika na Shirika la CAMFED, STUMAI KAGUNA alisema kwa upande wake amenufaika na Elimu ya kifikra pamoja na uchumi wake kwa ujumla ambapo anamiliki nyumba pamoja na miradi miwili ya Biashara ndogondogo wakati, aidha akawa asa wasichana wengine “Msikate tamaa,kwani kutoka kwenye familia masikini sio ndio mwisho wa mafanikio yako”.
Kwaupande wa MARIA KAMANDE alisema anamengi ya kujivunia kutoka CAMFED kama vile kuuona uthamani wake kwenye jamii na anazo nyumba mbili na kiwanja lakini pia anatunza na kuihudumia familia yake pamoja na watoto wa ndugu zake wawili,ikiwemo kuwasaidia kielimu,afya na mazibgira,hata hivyo “ukisaidiwa kumbuka kusaidia” alisema.
Bi,Wilbard akarejerea tuzo ya YIDAN walio tunukiwa mwishoni mwa mwezi September,mwaka huu,akasema tuzo hiyo niutambulisho mkubwa wa shirika la Camfed duniani kote kuhusu kazi zinazo fanywa na shirika hilo,kuhusu kumsaidia msichana anae toka kwenye mazingira magumu.
Shirika la CAMFED linahudumia vijana wa kike katika Nchi tano Barani Africa na kwamba malengo yake ni kuwafikia wasichana milioni tano ifikapo mwaka wa 2025,ilikuwasaidia kufikia ndoto zao kielimu,na kiuongozi.