Asasi ya kujitolea ya Home Start inayofanya kazi ya kutoa
huduma kwa Familia Changa zenye changamoto za malezi ya watoto ambao
hawajafikia Umri wa kusoma, imetoa mafunzo kwa wahudumu 12 ngazi ya jamii
Manispaa ya Morogoro tayari kuanza kazi ili kutengeneza usawa wa Maisha na
malezi Bora ngazi ya Familia.
Wahudumu hao wa familia waliopewa mafunzo katika ukumbi wa
Kilimo Manispaa ya Morogoro, watafanya kazi ya kusimamia Famili mbili kwa kila
mmoja ndani ya Mwaka mzima huku wakizitolea taarifa kwa mratibu wa Asasi, ambaye ataziwasilisha taarifa hizo kwenye Ofisi ya Maendeleo ya Jamii Manispaa ya Morogoro.
Akizindua Mafunzo hayo, Mkurugenzi Mtendaji wa Home Start
Tanzania Bi, ANNA TEMBA pamoja na mambo mengine pia ameiomba Serikali pamoja na
wadau kutoa ushirikiano kwa wahudumu walio pewa mafunzo ili kuzisaidia Familia
zenye changamoto ya Malezi.
‘’Hawa wahudumu
tuliowapatia mafunzo tunaamini wataenda kuleta mabadiliko kwenye ngazi za
familia, mimi kama Mkurugenzi wa Home Start naiomba Serikali na wadau kuweza
kuwapa ushirikiano ili kuifanikisha vema kazi ya kusaidia Familia’’ alisema
Anna Temba
VIPAUMBELE.
‘’kwa kweli kipaumbele kikubwa kwa Home Start tulichonacho ni Mtoto kwanza, tunatamani kuona kila
mhudumu kujua haki zote za mtoto na kuhakikisha jamii inazifahamu na kumlinda
Mtoto ipasavyo’’Anna.
LENGO LA ASASI.
Kaimu mratibu wa Home start Manispaa ya Morogoro, Delfina Thomas Pacho alisema ‘’Asasi yetu ya Home Start inafanya kazi kwenye jamii kuziepusha
Familia kusambaratika kutumia wahudumu walezi ambao wana uzoefu wa malezi ya
Familia na waliopokea mafunzo maalumu ya namna ya kuzisaidia familia zenye
changamoto ya malezi’’
Aidha Asasi hiyo ilianza Mwaka 2009 Nchini Tanzania hadi sasa imezisaidia Kaya zaidi ya 520 katika kuboresha malezi sahii ya
watoto na kutatua Migogoro ya Familia.
Miongoni mwa waliopokea mafunzo ni Sineno Faida na Anna William
walizungumza kwa niamba ya wenzao‘’katika mafunzo yetu ya leo nimejifundisha
katika Familia suala zima la malezi anatakiwa ahusike Baba na Mama kwahiyo wote
wawili wanatakiwa waisikie changamoto ya Mtoto na wampee nafasi ya kumsikiliza
na kuitatua changamoto ya Mtoto wao‘’ Sineno
Faida.
Na, Anna William akasema
‘’ yani mimi katika mafunzo ya leo nilichojifunza ni namna ya kuisaidia Jamii
katika kutatua migogoro na kutumia fursa zilizopo katika Jamii’’
Hata hivyo miongoni mwa mada zilizofundishwa katika mafunzo
hayo ni pamoja na wahudumu ngazi ya jamii kutambua haki za watoto, wajibu wa
muhudumu anayejitolea kwa Familia pamoja na kufanya tathmini baada ya kuisaidia
Familia.