Kwa mujibu wa Ripoti ya utafiti wa Hali ya Ukatili kwa watoto Shuleni
Tanzania Bara Ripoti ya mwaka 2020, kutoka Shirika la Haki Elimu Tanzania
inaeleza wapo watoto walioshindwa kutimiziwa mahitaji yao ya msingi na wazazi
au walezi wao ilihali walikua na uwezo huo.
Mahitaji ya msingi waliyopuuza wazazi/walezi kutimiza kwa watoto wao ni
matibabu ya kiafya, chakula, malazi, mavazi, Elimu, uangalizi mzuri wa watoto
nakadhalika.
Aidha wanafunzi waliohojiwa kama wazazi na walezi wao walipuuzia
kuwatimizia mahitaji yao na wakajibu ndio, walisema aina ya mahitaji
waliyoshindwa kutimiziwa kikamilifu ni, kutopata chakula cha kutosha na
vinywaji, kuvaa nguo chafu, kuvaa nguo zilizochanika, kuvaa viatu vidogo,
kutopelekwa hospitali pindi walipougua kumuona daktari au kupewa dawa lakini
pia hawakua wanapatiwa malezi mazuri.
Jedwali hapo chini linafafanua idadi ya wanafunzi walioshindwa kutimiziwa
mahitaji yao ya Msingi katika maeneo ya mijini, vijijini na katika Shule za
Msingi na Sekondari za Binafsi na za Serikali Tanzania Bara.
JINSI |
MSINGI |
SEKONDARI |
||||
Wavulana |
Wasichana |
Jumla |
Wavulana |
Wasichana |
Jumla |
|
Mjini |
205 (84.7%) |
229 (84.2%) |
434 (84.4%) |
60 (27.6%) |
51 (18.0%) |
111 (22.2%) |
Vijijini |
42 (21.0%) |
40 (19.5%) |
82 (20.2%) |
43 (24.2%) |
36 (15.9%) |
79 (19.5%) |
Shule za Binafisi |
12 (9.9%) |
18 (13.0%) |
30 (11.6%) |
22 (19.5%) |
32 (17.7%) |
54 (18.4%) |
Shule za Serikali |
67 (20.9%) |
65 (19.2%) |
132 (20.0%) |
81 (28.7%) |
55 (16.7%) |
136 (22.3%) |
Jumla |
79 (17.9%) |
83 (17.4%) |
162 (17.6%) |
103 (26.1%) |
87 (17.1%) |
190 (21.0%) |
Chanzo:
HakiElimu Tanzania.
Waandishi
wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad Rashid: [email protected]