Picha: Habari leo
Ripoti ya utafiti wa kujifunza iliyotolewa
Mwaka 2019 na Shirika la Uwezo Tanzania, inaonesha idadi kubwa ya watoto wa
darasa la 3 hadi la 7 bado hawana ujuzi wa msingi wa kusoma na kuhesabu. Na
kiwango cha ufaulu wa somo la Kiswahili
kwenye majaribio ya wanafunzi uliongezeka kwa wanafunzi wa Darasa la 6 ambapo
ufaulu ulikuwa wa 89%.
Hata hivyo Ripoti ya Uwezo
Tanzania inafafanua wastani wa ufaulu kwa Darasa la Tatu hadi Darasa la Saba
kwa somo la Kingereza uko chini ukilinganisha na ufaulu wa somo la Kiswahili
kwa madarasa hayo hayo, wakati huo Darasa la Tatu likifanya vibaya kutoa
matokeo yenye ufaulu wa chini kabisa kuliko Darasa la Saba kwa somo la Kingereza
kwanzia Mwaka 2011-2017.
Jedwali hapo chini linaeleza
zaidi kiwango cha ufaulu kwa majaribio ya Somo la Kingereza.
Darasa la Tatu |
12% |
12% |
19% |
21% |
13% |
14% |
15% |
Darasa la Saba |
48% |
53% |
56% |
56% |
48% |
47.5% |
47% |
Mwaka |
2011 |
2012 |
2013 |
2014 |
2015 |
2016 |
2017 |
Chanzo:
Uwezo Tanzania.
Waandishi
wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad Rashid: [email protected]