Kiwango
cha juu cha maambukizi ya Malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita ni asilimia
22.4% ilhali kiwango kidogo cha Malaria kipo katika Halmashauri ya Geita Mji ambayo
ni asilimia 10.4%, Kwa mujibu wa Ripoti ya Atlasi ya Malaria ngazi ya
Halmshauri iliyotolewa na Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS), Mwezi Agosti
2018.
Ripoti
ya Atlasi ya Malaria imebanisha, kiwango cha Malaria kwa watoto wenye umri wa
chini ya miaka mitano Mkoa wa Geita ni asilimia 17.3%, kiwango hiki cha Malaria
ni kikubwa kwa zaidi ya mara mbili ukilinganisha na wastani wa kitaifa wa
asilimia 7.3%.
Jedwali hapo chini linaonesha
asilimia za maambukizi ya Malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano kwa Halmashauri za Mkoa wa GEITA.
MKOA |
HALMASHAURI. |
ASILIMIA |
GEITA |
GEITA |
22.4% |
MBOGWE |
16.3% |
|
CHATO |
16.1% |
|
BUKOMBE |
15% |
|
NYANG’WALE |
12.3% |
|
GEITA MJI |
10.4% |
Chanzo: NBS
Waandishi wa Habari na wachambuzi
wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad Rashid: [email protected]