Kwa mujibu wa Ripoti ya Atlasi ya
Malaria ngazi ya Halmshauri iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Mwezi Agosti 2018 inaenesha, Kiwango
cha juu cha maambukizi ya Malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano ni asilimia 30.8 katika Halmashauri ya Wilaya ya Kakonko na kiwango cha
chini kipo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma ambayo ni asilimia 14.7.
kwa Mwaka 2017.
Aidha
Mkoa wa Kigoma una kiwango cha juu zaidi kuliko mikoa yote nchini katika
maambukizi ya
malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka mitano ikiwa ni asilimia 24.4,
kiwango hiki cha maambukizi ni kikubwa zaidi ya mara tatu ukilinganisha na
wastani wa kitaifa asilimia wa Asilimia 7.3.
Jedwali hapo chini linaonesha
asilimia za maambukizi ya Malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano kwa Halmashauri za Mkoa wa Kigoma.
MKOA |
HALMASHAURI |
ASILIMIA |
KIGOMA |
KAKONKO |
30.8% |
KASULU |
27.6% |
|
KIBONDO |
25.8% |
|
KIGOMA |
25.1% |
|
BUHINGWE |
24% |
|
KASULU MJI |
15.4% |
|
KIGOMA |
14.7% |
Chanzo: NBS
Waandishi wa Habari na wachambuzi
wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad Rashid: [email protected]