Ripoti ya Atlasi ya Malaria ngazi
ya Halmshauri iliyotolewa na Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS), Mwezi Agosti
2018 imetaja kiwango cha maambukizi ya Malaria kwa watoto wenye umri wa chini
ya miaka mitano katika Mkoa wa Kagera ni asilimia 15.4%, ikiwa
ni kubwa takribani mara mbili zaidi ukilinganisha na wastani wa kitaifa wa
asilimia 7.3%.
Kwa
mujibu wa Ripoti hiyo ya Atlasi ya Malaria, kiwango cha juu cha Malaria kipo
katika Halmashauri ya Wilaya yaMuleba
asilimia 19.4%, ilhali kiwango kidogo cha Malaria kipo katika
Halmashauri ya Manispaa ya Bukoba ambayo ni asilimia 3.5%.
Jedwali hapo chini linaonesha
asilimia za maambukizi ya Malaria kwa watoto wenye umri wa chini ya miaka
mitano kwa Halmashauri za Mkoa waKagera.
MKOA |
HALMASHAURI. |
ASILIMIA |
KAGERA |
MULEBA |
19.4% |
BIHARAMULO |
18.9% |
|
KYERWA |
16.7% |
|
NGARA |
16.2% |
|
KARAGWE |
14.9% |
|
BUKOBA |
10.6% |
|
MISSENYI |
7.1% |
|
BUKOBA |
3.5% |
Chanzo: NBS
Waandishi wa Habari na wachambuzi
wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad Rashid: [email protected]