Picha na Ipp media
Kwa mujibu wa ripoti ya kitabu cha hali ya uchumi wa
taifa katika mwaka 2020 kutoka Wizara ya Fedha na mipango, katika ukurasa wa
260 kipengele cha Lishe,
kinaeleza kuwa Mwaka 2020, Serikali iliendelea kutekeleza Mpango Jumuishi wa
Taifa wa Lishe wa (2016/17 – 2020/21) ili kukabiliana na athari za lishe duni
na kuimarisha ukuaji mzuri wa mwili na akili kwa mtoto.
Katika
kipindi hicho cha Mwaka 2020/2021, zaidi ya asilimia 90% ya watoto milioni 9
walio chini ya umri wa miaka mitano walipatiwa matone ya Vitamini A.
Aidha,
asilimia 91.3% ya watoto waliozaliwa katika vituo vya kutolea huduma za Afya Mwaka
2020 walinyonyeshwa ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa ikilinganishwa na
asilimia 89.9% walionyonyeshwa mwaka 2019. Vile vile, asilimia 5.6% ya watoto
walizaliwa na uzito pungufu mwaka 2020 ikilinganishwa na asilimia 5.7% ya
watoto Mwaka 2019.
Kwa upande
mwingine, asilimia 0.9% ya wajawazito waliopimwa wingi wa damu katika hudhurio
la kwanza walikuwa na upungufu mkubwa wa damu ikilinganishwa na asilimia 1.4%
ya Mwaka 2019.
Chanzo:
Wizara ya Fedha na Mipango.
Waandishi
wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad
Rashid: [email protected]