Mwaka 2020, idadi ya vituo
vilivyo karabatiwa kwa ajili ya kutoa huduma ya upasuaji wa kumtoa mtoto
tumboni iliongezeka na kufikia 487
mwaka 2020 kutoka vituo 352 mwaka
2019, sawa na ongezeko la asilimia 38.4,
Kwa mujibu wa ripoti ya kitabu cha hali ya uchumi wa taifa katika mwaka 2020.
Ongezeko la vituo hivyo vya
Afya ilichangiwa na jitihada za Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta
binafsi kuendelea kuboresha miundombinu ya afya.
Aidha, idadi ya vituo vya
kutolea huduma za uchunguzi wa mabadiliko ya awali ya Saratani iliongezeka na
kufikia vituo 746 mwaka 2020 kutoka
vituo 624 Mwaka 2019, ambapo
wanawake 533,780 walifanyiwa
uchunguzi ikilinganishwa wanawake 413,851waliofanyiwa
uchunguzi Mwaka 2019.
Chanzo:
Wizara ya Fedha na Mipango.
Waandishi
wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad
Rashid: [email protected]