Ripoti ya kitabu cha hali ya
uchumi wa Taifa mwaka 2020, katika kipengele cha Afya ya Uzazi na Mtoto Mwaka
2020, idadi ya wajawazito 2,394,736
walihudhuria kliniki ikilinganishwa na wajawazito 2,320,559 mwaka 2019, sawa na ongezeko la asilimia 3.2.
Aidha, asilimia 37.7 ya wajawazito walifanya hudhurio la kwanza kabla ya majuma 12 mwaka 2020 ikilinganishwa na
asilimia 34 mwaka 2019.
Wajawazito waliohudhuria
kliniki angalau mara nne waliongezeka kutoka asilimia 80.4 mwaka 2019 hadi asilimia 90.1
mwaka 2020.
IDADI YA WAJAWAZITO |
2019 |
2020 |
|
2,320,559 |
2,394,736 |
MAHUDHURIO KLINIKI YA KWANZA |
34% |
37.7% |
MAHUDHURIO KLINIKI MARA NNE |
80.4% |
90.1% |
Chanzo:
Wizara ya Fedha na Mipango.
Waandishi
wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad
Rashid: [email protected]