Kwa mujibu wa ripoti ya kitabu
cha hali ya uchumi wa Taifa katika Mwaka 2020
Chanjo ya PENTA-3 na Surua
rubella zilitolewa kwa (asilimia 98).
Rota2 ni (asilimia 91.5).
OPV 1 (asilimia 84) na
OPV 2 (asilimia 75).
Chanjo hizo hutolewa kwa lengo
la kuzuia magonjwa ya kupooza, kuharisha, pepopunda, pneumonia, homa ya
ini, homa ya uti wa mgongo, surua, polio na dondakoo kwa watoto walio chini ya
mwaka mmoja.
Aidha, Tanzania imeendelea
kutoa chanjo hizo ili kukidhia vigezo vya Shirika la Afya Duniani vinavyotaka
nchi kuhakikisha kuwa zaidi ya asilimia 90 ya watoto wa chini ya mwaka mmoja
wanapata chanjo.
Chanzo:
Wizara ya Fedha na Mipango.
Waandishi
wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad Rashid: [email protected]