Mwaka 2020, Serikali ilisajili
vituo 134 vya kulelea watoto wadogo
mchana ikilinganishwa na vituo 373
mwaka 2019 na kufanya jumla ya vituo vilivyosajiliwa kufikia 1,677. Katika kipindi hicho, jumla ya
watoto 163,394 (wavulana 85,175 na wasichana 78,219) waliandikishwa ikilinganishwa
na watoto 159,479 (wavulana 82,539 na wasichana 76,940) mwaka 2019, sawa na ongezeko la
asilimia 2.5.
Hili ilitokana na kuongezeka
kwa mwamko wa wazazi kuandikisha watoto wadogo kulelewa katika vituo. Aidha,
idadi ya walezi wa watoto katika vituo vya kulelea watoto wadogo mchana
iliongezeka na kufikia walezi 2,878
mwaka 2020 kutoka walezi 2,563 mwaka
2019. Ongezeko hili linatokana kuongezeka kwa idadi ya vituo vya kulea watoto
wadogo mchana.
Chanzo:
Kitabu cha hali ya Uchumi wa Taifa katika Mwaka 2020.
Waandishi
wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad
Rashid: [email protected]