Kitabu cha hali ya Uchumi wa Taifa cha Mwaka 2020,kinabaisha
kuwa Serikali ilitoa huduma za msingi pamoja na huduma za msaada wa kisheria
kwa watoto walio katika mkinzano na sheria katika mahabusu za watoto za Mbeya,
Kilimanjaro, Tanga, Arusha na Dar es Salaam.
Katika kipindi hicho, jumla ya watoto 138 (wasichana 18 na
wavulana 120) walio katika mkinzano na sheria walipata huduma za chakula,
malazi, mavazi, huduma za matibabu na elimu ikilinganishwa na watoto 250
(wasichana 19 na wavulana 231) mwaka 2019.
Aidha, jumla ya watoto 78 (wasichana 5 na wavulana 73)
waliokuwa katika mkinzano na sheria
walichepushwa kutoka katika mfumo rasmi wa haki jinai kwa
kuwarekebisha tabia na kuwaunganisha na familia zao mwaka 2020 ikilinganishwa
na watoto 148 (wasichana 59 na wavulana 89) mwaka 2019.
Watoto walio katika |
Mwaka |
Wasichana |
Wavulana |
Jumla |
2020 |
18 |
120 |
138 |
|
2019 |
19 |
231 |
250 |
|
Watoto waliochepushwa |
2020 |
5 |
73 |
78 |
2019 |
59 |
89 |
148 |
|
|
|
|
|
Chanzo:
Kitabu cha hali ya Uchumi wa Taifa katika Mwaka 2020.
Waandishi
wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad Rashid: [email protected]