Ripoti ya takwimu za elimu ya mwaka 2020 iliotolewa
na Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa, inaonesha idadi ya
wanafunzi yatima kwa shule za awali za
serikali kwa halmashauri na Mkoa nchini, ambapo jumala ya wanafunzi wa Darasa
la Awali walio andikishwa kwa mwaka 2020 ni 1,278,886 kwa Shule zote
za Serikali Tanzania bara.
Mkoa wa Mwanza
unaongoza kwa kuwa na wanafunzi wengi yatima 95697 wa darasa la
awali, ukifuatiwa na Mkoa wa Kagera kwakuandikisha
wanafunzi 84261
Aidha Ripoti ya Best 2020, imeutaja Mkoa wa Katavi
kuwa na idadi ndogo zaidi kuandikisha wanafunzi
yatima 18619 wa Darasa la Awali.
Kwangazi ya halmashauri inayo ongoza kwa kuandikisha
wanafunzi wengi yatima ni halmashauri ya Muleba Mkoani Kagera iliandikisha
wanafunzi 18441, ikifuatiwa na
halmashauri ya Kwimba Mkoani Mwanza
iliandikisha wanafunzi 15069. Na
halmashauri ya Mlele Mkoa wa Katavi iliandikisha wanafunzi 1230 ni wachache kuliko halmashauri
zote Tanzania Bara.
Chanzo:
Kitabu cha hali ya Uchumi wa Taifa katika Mwaka 2020.
Waandishi
wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad
Rashid: [email protected]