Ripoti ya takwimu za elimu ya mwaka 2020 iliotolewa
na Ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa, inaonesha idadi ya
wanafunzi wanaotoka katika mazingira magumu kwa shule za Msingi za serikali na binafisi
kwa halmashauri na Mkoa nchini, ambapo jumala ya wanafunzi wa Darasa la kwanza
walio andikishwa kwa mwaka 2020 ni 10,925,896 kwa Shule zote za Serikali
na binafisi Tanzania bara.
Mkoa wa Mwanza
unaongoza kuandikisha wanafunzi wengi wanao toka mazingira magumu 797539 wa darasa la awali, huku
Mkoa wa Dar es Salaam ukiandikisha
wanafunzi 706494.
Aidha Ripoti ya Best 2020, imeutaja Mkoa wa Njombe kuwa imeandikisha idadi ndogo zaidi ya wanafunzi
wanaotoka mazingira magumu 168722 wa Darasa la kwanza.
Chanzo:
Kitabu cha Takwimu za Elimu ya Mwaka 2020.
Waandishi
wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad Rashid: [email protected]