Kutoka katika Ripoti ya utafiti juu ya upataji Elimu ya awali kwa watoto wenye ulemavu Tanzania
Bara , iliyozinduliwa sepemba 14, 2021 na Shirika la Haki Elimu
Tanzania, imebainisha Utafiti
uliotaka kuelewa ufadhili wa watoto wa shule ya awali wenye ulemavu, mahojiano waliyofanyiwa
na maofisa wa wizara miongoni mwao kutoka -TAMISEMI wamefichua kuwa hakukuwa na
fedha maalum kwa ajili ya shule ya awali kwa watoto wenye ulemavu.
Kwa kuwa elimu ya shule ya awali ni sehemu
ya elimu ya msingi, hivyo hufadhiliwa kupitia ruzuku ya mwanafunzi, ambapo TZS
10,000 hutengwa kwa kila mwanafunzi. Kuhusu suala la kiasi kinachotengwa, 60% hutarajiwa kwenda moja kwa moja shuleni na
40% iliyobaki inatumika kwa vitabu vya kiada.
Matokeo kutoka kwa wakuu wa shule,
walifichua kuwa ruzuku ya mwanafunzi iliyopokelewa haikukidhi elimu ya awali, Kando
na hayo, ruzuku ya mwanafunzi haitegemei usawa, Kwa hivyo hakukuwa na ufadhili maalum
kwa shule ya awali wanafunzi wa shule kutoka serikalini.
Wakuu wa shule waliulizwa zaidi kama kulikuwa na ufadhili
wa kusaidia wanafunzi wa shule za awali wenye ulemavu katika mazingira ya
elimu-jumuishi.
Takriban 72.3%
wakuu wa shule waliohojiwa walikiri kuwa hawakua na fedha za ziada kusaidia
wanafunzi wenye ulemavu lakini Kati yao wakuu wachache wa shule walioripotiwa
kuwa na ziada ya fedha, vyanzo vya ufadhili vilitokana na michango ya wazazi
(30.4%), ufadhili kutoka kwa wafadhili (56.5%), kujitegemea shuleni (39.1%) na
vyanzo vingine (34.8%).
Haki Elimu
Waandishi
wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad Rashid: [email protected]