Ripoti ya utafiti juu ya upataji Elimu ya awali kwa
watoto wenye ulemavu Tanzania Bara , iliyozinduliwa sepemba 14, 2021 na Shirika la
Haki Elimu Tanzania, imebainisha hali ilivyo kuhusu vyoo kwa watoto wenye
ulemavu wa darasa la awali Nchini.
Katika utafiti huo Shule nyingi zina vyoo
vya shimo, ingawa katika hali tofauti baadhi ya vyoo viko katika hali nzuri wakati
vingine haviko kwenye hali nzuri.
Kwenye Shule zote zilizo tembelewa takriban
75% ya shule hizo hazina vyoo vya
watoto wenye ulemavu,watoto hao wenye ulemavu wamekuwa wakishiriki vyoo na
watoto wengine wasio wenye ulemavu.
Ni 15% tu ya shule zina vyoo vinavyo kidhi mahitaji ya watoto wenye
ulemavu,na takriban 10% ya shule zina
vyoo vya watoto wenye ulemavu ingawa hazikubadilishwa ili kukidhi mahitaji ya
watoto wenye ulemavu, baadhi ya shule ziligundulika kuwa na vyoo
vilivyoboreshwa lakini havitumiki.
Kati ya shule za msingi zilizotembelewa
katika Manispaa ya Tanga, kulikuwa na vyoo maalum vilivyotengwa kwa ajili ya
watoto wenye ulemavu,
ingawa havitumiki, badala yake, vilitumika kama chumba cha makopo matupu ya
maji.
Vile vile, katika shule nyingine vyoo vya
watoto wenye ulemavu vilikuwepo na viko katika hali nzuri lakini havikutumika
kwani walikuwa wamefungwa kila wakati.
Aidha ripoti hiyo ya utafiti ilibainisha
kuwa asilimia 70 ya shule
zilizotembelewa hazikuwa na vyoo vilivyotengwa kwa wanafunzi wa darasa la
awali.
Chanzo: Haki Elimu
Waandishi
wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad Rashid: [email protected]