Kwa mujibu wa Ripoti ya utafiti juu ya
upataji Elimu ya awali kwa watoto wenye ulemavu Tanzania Bara
, iliyozinduliwa sepemba 14, 2021na Shirika la
Haki Elimu Tanzania, inaonesha kuwa Shule za Msingi nyingi
zilizotembelewa hazijaandaliwa vyema kusaidia upatikanaji wa usawa na ushiriki
wa watoto wenye ulemavu katika elimu ya awali.
Karibu 66% ya shule zilizo tembelewa zina
njia zenye kokoto na mawe, utafiti huo uligundua kuwa ni 16% tu ya Shule
zilikuwa na njia ambazo zilikuwa katika hali nzuri.
Aidha 35% ya shule hazina Barabara hata kidogo, na
maeneo madarasa maalum yaliyotengwa kwa ajili ya watoto wenye ulemavu, yatakayo
wawezesha watoto kufikia kiurahisi.
Chanzo: Ripoti ya Utafiti juu ya upataji Elimu ya awali kwa
watoto wenye ulemavu Tanzania Bara 2021.
Waandishi
wa Habari na wachambuzi wa Takwimu hizi ni: –
John Kabambala: [email protected]
Hamad Rashid: [email protected]