Herriet Mkaanga Mkurugenzi wa Taasisi ya My Health Foundation.
Kufuatia waraka wa Serikali ulioelekeza wanafunzi wa
kike waliopata ujauzito warejee shule katika mfumo rasmi baada ya kujifungua
wadau wa Elimu nchini wameipongeza Serikali kwa hatua hiyo.
Herriet Mkaanga, mwanaharakati wa watoto wa kike na
Mkurugenzi wa Shirika la My Health Foundation ambalo limekua likipigania suala hili kwa muda
mrefu, aliishukuru Serikali kwa hatua
hiyo na kutoa maoni yake kuwa wapatiwe Elimu ya saikolojia kabla ya kurejeshwa
Shule ili wakafanye vizuri zaidi.
Fika Fahari Shop kwa huduma zaidi za malighafi ya mbalimbali ya kutengenezea Bidhaa.
Mkaanga pia alisema juhudi nyingine zinazotakiwa
kuchukuliwa dhidi yao ni kuwezesha mazingira yao ya kujifunzia ili wasiingie
tena katika ushawishi wa kupata ujauzito ikiwemo, kuwasaidia taulo za kike,
vyakula kwa Shule zenye mabweni.
watoto wakiwa kwenye sare kutoka kituo cha kulelea watoto Step up day care center Sabasaba Morogroro. mawasiliano yao: 0756557228.
kwa mujibu wa Takwimu za Elimu ripoti ya Best 2020
inaeleza jumla ya idadi ya wanafunzi wa kike 1,135 sawa na 0.7% walipata
ujauzito katika Shule za Msingi, ilhali shule za Sekondari walikua 5,398 sawa
5.5% mwaka 2019.
Na
John Kabambala.