Deodatus Balile Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri Tanzania (TEF)
Kufuatia waraka wa Serikali ulioelekeza wanafunzi wa
kike waliopata ujauzito warejee shule katika mfumo rasmi baada ya kujifungua, wadau wa Elimu nchini wameipongeza Serikali kwa hatua hiyo.
Deodatus Balile, Mwenyekiti wa Jukwaa la wahariri
Tanzania -TEF ambalo limekua likipigania suala hili kwa muda mrefu, ameipongeza
Serikali kwa hatua hiyo na kuahidi kuwapambania watoto siku hadi siku kupitia
miradi mbalimbali wanayotekeleza kwa ushirikiano na Shirika la umoja wa mataifa
la kuhudumia watoto UNICEF.
Katika hatua nyingine amewatahadhalisha wanafunzi wa
kike kutojihusisha na ngono hadi wakati wao wa ndoa utakapofika kwa ajili ya
manufaa yao na taifa kwa ujumla, Balile ameyasemahayo wakati wa mahojiano maalumu na waandishi wa habari kutoka Tanzania Kids Time(TKT/UN REDIO) mjini Morogoro mwishoni mwa mwezi Novemba.
Kwa mujibu wa Takwimu za Elimu ripoti ya Best 2020
inaeleza jumla ya idadi ya wanafunzi wa kike 1,135 sawa na 0.7% walipata
ujauzito katika Shule za Msingi, ilhali shule za Sekondari walikua 5,398 sawa
5.5% mwaka 2019.
Na
Hamad Rashid