Sameer Twaha ambaye ni mtoto wa Bondia anayefanya
vizuri nchini Tanzania amepewa ubalozi wa kuvitangaza vituo vya kulelea watoto
mchana, vya Green Apple day care Centers vilivyopo Kata ya Kilakala, Kata ya
Mazimbu na Kata ya Mkundi katika Halmashauri ya Manispaa ya Morogoro ubalozi
utakaodumu kwa kwa muda wa miaka miwili.
Bondia Twaha Kiduku akisani mikataba ya ubalozi wa Mwanae Sameer Twaha.
Akizungumza katika mkutano na waandishi wa Habari
uliofanyika katika Kituo cha kata ya Kilakala, Mkurugenzi wa Green Apple day
care, Mwajabu Kusaga alisema “mimi kama
Mkurugenzi wa Gree Apple na mdau wa
watoto tumeona Sameer awe Balozi wa vituo vyetu vya day care ni kwanini Sameer,
kwasababu kama ambavyo Baba yake Sameer kwa kipaji alichonacho na sisi pia
Green Apple tunaamini kwenye vipaji vya watoto, sasa tukaona kwa kumtumia
Sameer na nembo ya Baba yake hivyo ni mudada wa Sameer kuweza kuhamasisha watoto
wengine waweze kujihusisha katika vipaji mbalimbali walivyonavyo ikiwemo Ngumi’’
ubalozi wa mtoto wake akishukuru uongozi wa Shule za Green Apple kwa kumchagua
mtoto wake kuwa balozi wa Green Apple day care.
“Nipende kuwaambia watu wa Morogoro wenye watoto wao
wa umri kama huu kuwaleta watoto wao katika vituo vya Green Apple day care
centers kikukweli mazingira ni mazuri na kuna utulivu” alisema Bondia Twaha
Rubaha maarufu Twaha kiduku.
Aishan Makeki ni watengenezaji wa Keki bora wanakukaribisha katika Ofisi yao iliyopo Masika Morogoro kwa mahitaji ya Keki popote ulipo watakuhudumia piga simu namba: 0713835087 au 0625900801.
Miongoni mwa waliohudhuria katika mkutano huo wa
waandishi wa Habari ni Mzazi aliyejitamburisha kwa jina moja la Rahma ambaye ni
mzazi wa mtoto Najma Ally anayesoma katika kituo cha Green Apple Kilakala,
alisema mtoto wake alivyompeleka hakuwa afahamu hata kuzungumza vizuri lakini
sasa anaweza hata kutaja majina yake na kujitamburisha kwa kiingereza pamoja na
kujiamini kwake kumeongezeka.
Rahma aliongeza kuwa “ mwanangu katika mtihani wa
mwezi wa sita alishika nafasi ya kwanza na mtihani wa mwezi wa kumi na mbili amekua
wa pili, kwa hiyo naweza sema kwamba Green Apple ni Shule nzuri sana na walimu
wake ni rafiki pia mtoto anakua na hamasa ya kwenda Shule”