kulelea watoto mchana yaliyofanyika katika kituo hicho kilichopo Mtaa wa Reli
Kata ya Mazimbu, Mgeni Rasmi wa hafla hiyo Mwenyekiti wa Mtaa wa Reli Henry
Sebastian Mapunda alisema, wazazi na walezi ni vyema kuwapeleka watoto wao
Valentine day care ili wakapate malezi bora kulingana umri wao.
Keki kama hizo utazipata kwa Aishan Makeki wako masika kituo cha daladala Manispaa ya Morogoro, wanapokea oda zote wasiliana nao kupitia: +255 713 835 087.
Kwa upande wa Mwalimu mlezi wa Valentine day care
Salome Mbowe alisema, “watoto wananipenda na mimi ninawapenda”.
Salome aliongeza kwa kuwapongeza wanafunzi wake Benedict
Sanga na Naurath Simba kwa uelewa mzuri walionao akiahidi kuwa amejipanga
kuongeza ujuzi zaidi kwa Mwaka wa 2022 akiamini watoto watakua wengi zaidi ya
Mwaka huu wa 2021.
Darasa la Ujasiriamali likiwa linaendelea katika Chuo cha Victory Morogoro, ambao sasa wanaendelea kupokea wanafunzi kwa ajili ya muhula mwingine wa masomo, Chuo kipo Sabasaba Jengo la CCM Mkoa Ghoroga ya Tatu, mawasiliano yao ni: +255 715 176 176.
Tanzania kids time ilizungumza na Mzazi Suzana
Mzumbwe ambaye ni Mama wa Mwanafunzi Benedict Sanga aliyehitimu Elimu ya
Chekechea, alisema “mtoto wangu amesoma hapa na leo amehitimu, kwakweli ni
Shule ambayo wamemlea vizuri, kitaaluma yuko vizuri, Mwalimu wake yuko vizuri
maendeleo ya mwanangu nimeyapenda yako vizuri na nina uhakika Shule atakayoenda
atafanya vizuri” alisema Suzana Mzumbwe.
Mkurugenzi wa Valentine day care Center Mwalimu
Margareth Valentine alisema, Kituo chake kinapokea watoto wa kuanzia umri wa
Mwaka mmoja hadi miaka mitano hivyo wazazi na walezi wanaosumbuka kutafuta binti
wa kazi za nyumbani sasa wamepata suluhisho.
Bi Margareth aliongeza kuwa, wanapokea watoto wa
aina mbili, wanaotoka sa sita mchana na wanaotoka sa kumi jioni.
Kituo cha kulelea watoto mchana Valentine day care
kimefanya Mahafali yake ya pili ambapo watoto waiwili wamehitimu Benedict Sanga
na Naurath Simba.
Na John Kabambala.