Shine Up Day Care Center ni kati ya kituo cha
kulelea watoto mchana kilichopo mtaa wa mkwajuni kata ya Mindu ndani ya
Manispaa ya Morogoro, kituo hiki kilianzishwa mwaka 2020, na Mwaka 2021
kimetimiza miaka miwili na kufanya Mahafali yake ya pili tangu kuanzishwa kwake
mwaka 2020.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa kituo hicho Bi, Upendo Mchau kupitia
risala iliondaliwa kwa mgeni Rasimi alisema mwaka 2021 wamehitimu watoto kumi na
saba (17) ambao wote wamefauru kujiunga na shule ya msingi kuanza Darasa la
kwanza mwaka 2022 jambo ambalo ni miongoni mwa mafanikio ya kituo ikiwa ni
pamoja na kutoa malezi bora kwa watoto.
Afya ni mtaji wa kwanza katika maisha, ilikufanya yote uyatakayo ni lazima uwe na afya bora,Fukang Health Care niwataalamu wa kutibu magonjwa ya binadamu, wanapatikana Morogoro unaweza kuwapigia simu namba. 0758903458.
Mgeni Rasmi wa Mahafali ndg. Razack Seleman akiijibu
Risala hiyo alianza kwa kuwapongeza vijana wenzake wamiliki wa kituo kwa kuanzisha
kituo cha kulelea watoto ambacho kimekuwa msaada kwa jamii ya watu wa
Kata ya Mindu, na kuwa asa wazazi na walezi kufanya uchaguzi sahihi kuwapeleka
watoto wao Shine up day care kupata Elimu na malezi yaliyo bora.
Akizungumza kwa niaba ya wazazi, Mlezi wa Shine up
day care center Mchungaji Katana Mwangome alisema Kituo cha Shine up dad care kimebadilisha
maadili ya watoto kuwa mazuri nidham yao ikiongezeka hivyo wazazi wamekua na matumaini
makubwa ya kuwapata viongozi bora wa Taifa la kesho kupitia Shine up day care
Center.
Picha zenye ubora,Video zenye ubora na matangazo yenye ubora zaidi huandaliwa na vifaa vyenye ubora zaidi, kwa maana ya Camera za kisasa, unazipata Morogoro kwa ASAK TECHNOLOGY, sim 0658251765.
Miongoni mwa wageni wa heshima waliohudhuria
Mahafali ya Shine up day care center ni Diwani wa Kata ya Mindu Mheshimiwa
Zuberi Mkaraboko na Mwenyekiti wa Mtaa wa Mkwajuni Bwana Juma Balali.