Tarehe 11/12/2021 yalifanyika Mahafali ya kuwaaga wanafunzi 45 wahitimu wa Elimu ya awali katika kituo cha kulelea watoto mchana Mery Children day care, mafahali yaliyofanyika katika ukumbi wa Washington Pub uliopo Kata ya Sabasaba Manispaa ya Morogoro, huku wazazi, na wageni waalikwa wakihudhuria kwa wingi.
Mgeni Rasmi katika Mahafali hayo alikua Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Morogoro, Dorothy Mwamsiku ambaye alitumia mkusanyiko huo kuwa asa wanawake kutorudi nyuma katika malezi ya watoto wao ikiwemo kutimiza wajibu wao katika suala la Elimu Ya Mtoto ili baadae waweze kufaidi matunda.
Bi, Dorothy aliongeza kuwa wanawake wengi wamekua wakiwaachia wanaume matunzo ya Mtoto hususani suala la mahitaji ya msingi katika Elimu.
Aidha Dorothy aliwapongeza walimu walezi na uongozi wa kituo cha Mery Children day care kwa malezi bora wanayowapatia watoto na kuwahimiza wazazi wengine kuwapeleka watoto wao ili wakapate malezi sahihi Mery Children day care.
Akiunga mkono Hotuba ya Mgeni Rasmi, MmoJa wa wazazi aliyehudhuria Mahafali hayo, Anthonia Emmanuel alisema ni kweli wanawake wengi hujisahau katika matunzo ya watoto wao ikiwemo kusimamia imara haki ya Mtoto kupata Elimu wakiwaachia wanaume peke yao.
Nae mkuu wa kituo cha Mery Children day care, Mwalimu Maria Sabas maarufu, Madam Merry alisema wanajivunia kuwa na mafaniko makubwa ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya watoto katika kituo chao tangu kianzishwe miaka saba iliyopita wakianza na watoto saba na hadi sasa wakiwa na watoto zaidi ya 130.
Alisema wanapokea watoto wa kuanzia umri wa miaka miwili na nusu hadi miaka mitano na kuwapatia malezi na Elimu bora kulingana na taaluma bora za walimu walezi waliyopo kituoni hapo.
Jumla ya watoto 45 walihitimu Elimu yao ya awali, wakitunukiwa Vyeti na zawadi mbalimbali, ambao mwezi wa kwanza mwaka 2022 wanataraji kujiunga Elimu ya Msingi kwa ajili ya masomo ya Darasa la kwanza.
Na Hamad Rashid.