Pichani ni Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro Bi, Jissica Kagunila
Matukio ya Mimba za utotoni yaliyoripotiwa Ofisi ya
Afisa ustawi wa Jamii Mkoa wa Morogoro, yaliongezeka kutoka 800 mwaka 2019/2020
hadi kufikia zaidi ya 1200 Mwaka 2020/2021.
Akithibitisha Takwimu hizo Afisa usatawi wa Jamii Mkoa
wa Morogoro Bi, Jessica Kagunila, alisema sababu ya Mimba za utotoni kuongezeka
inachangiwa na Mila na Desturi za Mkoa huo pamoja na malezi yasiyo mazuri ya
watoto.
“Tukianza
kwa Mwaka 2019/2020 matukio ya mimba za utotoni yaliyoripotiwa ni 800 lakini
tukija kwa Mwaka 2020/2021 yameongezeka hadi kufikia zaidi ya 120, hii ni
kutokana na Mila na desturi na malezi yasiyo mazuri kwa upande wa walezi na
wazazi’’ alisema Jessica Kagunila
Kwa mujibu wa Ofisi ya muendesha Mashtaka Mkoa wa
Morogoro DPP, matukio ya mimba za utotoni ambayo kisheria huitwa matukio ya
ubakaji yanaongezeka kutokana na watuhumiwa wa makossa hayo kutoa Rushwa kwa
waathirika na kesi kukosa ushahidi Mahakamani, alisema kaimu uendesha mashtaka
wa Mkoa wa Morogoro Flora Massawe.
“Inatokea
mara nyingi mahakamani, mashahidi wengi ambao ni wahanga watoto wanakuja
kugeuka yaani ule ushahidi waliotoa Polisi kwamba wamefanyiwa kitendoi cha
ubakaji na flani wakifika mahakamani wanakuja kukataa, na hii tumebaini
kutokana na wazazi kuridhia kufanya makubaliano na mtuhumiwa kuna kiasi cha
Pesa wanalipana, basi huku kesi zinaharibika’’ alisema Flora Massawe
Afisa ustawi wa Mkoa wa Morogoro Bi, Jessica alieleza
namna ambavyo watazidi kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha matukio
ya Mimba na Ndoa za utotoni yanapungua.
Bi,
Jessica alisema “Elimu sio suala la ustawi wa Jamii peke
yake, maendeleo ya Jamii na wadau wengine wa Elimu tutaendelea kushirikiana kuzunguka
shuleni kutoa elimu na hata kuwafikia wazazi kadri tutakavyoweza pamoja na
walimu ambao wanakaa muda mrefu na watoto’’
Katika kumulikia juhudi za Sekta binafsi kushirikiana
na Serikali juu ya kutokomeza Mimba za utotoni Mkoa wa Morogoro, Tanzania kids
time ilizungumza na Mratibu wa Miradi Evarist Momburi, kutoka Shirika la SAWA
WANAWAKE TAZNANIA lililojikita katika kusimamia ulizi wa Mtoto na utoaji Elimu
jumuishi kwa Shule za Msingi, ili kusikia maoni yake pamoja na juhudi zao
katika hili.
“kama
tunataka tupunguze hili tatizo la Mimba za utotoni, dawa yake ni kujenga mabweni
na kujenga Shule shikizi ambazo zitasaidia kupunguza ule umbali wa mwanafunzi
kutembea kuifata Shule ilipo, na hili tulifanya utafiti tukagundua watoto wengi
walikuwa wanakatiza masomo kwa sababu walikua wanapata changamoto ya umbali kuifata Shule ilipo’’
Alisema katika Mkoa wa Morogoro Shirika la, SAWA
WANAWAKE TANZANIA tayari limeshaboresha mabweni ya wasichana katika Shule za
Sekondari za DOMA na MVOMERO na Mwaka 2022 wamejipanga kuifikia Shule ya
Sekondari WAMI DAKAWA kupitia Mradi wake wa TUWALINDE WATOTO.