Nchini Tanzania umri wa balehe ni kipindi
kinachoambatana na hatari zaidi kwa wasichana, hasa kwa wale waishio katika
mazingira magumu, jambo linaloonyesha umuhimu wa kuongeza na kuendeleza
uimarishaji wa uelimishaji kuhusu usawa wa kijinsia, haki na maendeleo yao ya
wasichana.
Ili kuisaidia Serikali katika kuelimisha kundi hili
lililopo kwenye hatari zaidi, vyama vya kiraia, jamii, wazazi, walezi, viongozi
wa dini, viongozi wa kimila, wasichana na wavulana wenyewe wanapaswa kushiriki
kikamilifu kila mmoja kwa sehemu yake, ili kukabiliana na changamoto zinazo
wazunguka wasichana.
Mkoani
Morogoro nimezungumza na baadhi ya wasichana walio katika umri wa rika balehe,
kusikia wanafahamu nini kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia, Bakita Andrea mkazi wa Manispaa ya Morogoro
ni msichana mwenye umri wa miaka kumi natatu (13) mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya msingi saba saba “A” iliopo Manispaa ya Morogoro,
anaelezea vitendo vya ukatili.
“Ukatili ni unyanyasaji wa kijinsia
kwakuwafanyisha kazi ngumu zisizo endana na umri wao kuwapiga, kuwanyanyasa na
kuwatenga, ukatili huwakuta sana watoto wakike, wengine hufanyiwa ukatili na
wazazi wao, ndugu zao jamaa na marafiki n ahata walimu wao. Nakumbuka juzijuzi
shule ya Mazimbu alijinyonga mwanafunzi wa darasa la tano kwa kufanyiwa ukatili
na babayake aliharibika sehemu zake za siri kwasababu alikuwa akibakwa na
babayake” Amesema.
Aidha Bakita anasema madhara yanayoweza
kujitokeza kwa binti alie fanyiwa ukatili, “Ukatili
wa namna hiyo huleta madhara kwa mtoto wakike kwa kumuharibia sehemu za siri
nakumfanya awe hayupo makini darasani kwa sababu akiwa darasani mudawote nimtu
wakuwaza nikirudi nyumbani usiku kazi kwa baba ataanza kuni fanyia vitendo vya
ukatili”.
Bakita akapaza sauti yake kwaniaba ya
wasichana wengine kwa Serikali kuhusu watu wanao fanya vitendo vya ukatili
dhidi ya watoto wakike, “Serikali
ikomeshe vitendo vya ukatili na itoe adhabu kali kwa wale wanao wafanyia watu
vitendo vya ukatili”.
Hata hivyo Maria Mussa yeye ni mwanafunzi wa
darasa la saba shule ya msingi Uhuru iliopo katika Manispaa ya Morogoro,
anaeleza anayo yafahamu juu ya ukatili wanao fanyiwa watoto hasa wakike.
“Nakumbuka kulikuwa na watoto watatu waliokuwa
wakiishi na bibi, babu na binamu yao, kumbe binamu yao akawa kila siku anaingia
kwenye chumba cha hao watoto watu nyakati za usiku wakiwa wamelala na kuwa
fanyia ukatili kwa kuwarawiti na kuwambia wakipiga kelele nawaua”.
Maria akatoa ushauri kwa jamii hususani
wazazi, “Wazazi wawe wanawalinda watoto
na wawe wanakaa nao watoto karibu wenyewe kwa sababu watoto wakienda kulelewa
na watu wengine ndio wanawafanyia ukatili” Amesema.
John Kabambala-TKT/UnnewsKiswahili-Morogoro.