By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
Tanzania Kids Time
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Mazingira
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Wasiliana Nasi
Reading: WAZAZI NI MUDA SASA WAKUWAFUNDISHA ELIMU YA AFYA YA UZAZI VIJANA BALEHE ILI KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA VVU
Share
Notification Show More
Latest News
Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
TANZANIA WILL HOST CIGOFA4 TO FIND CONCRETE SOLUTIONS FOR YOUTH LAND QUESTIONS
Editor's Pick
Aa
Aa
Tanzania Kids Time
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
  • Contact
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Tanzania Kids Time > Blog > Afya > WAZAZI NI MUDA SASA WAKUWAFUNDISHA ELIMU YA AFYA YA UZAZI VIJANA BALEHE ILI KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA VVU
AfyaElimuUchambuzi na TakwimuUkatiliUmasikini

WAZAZI NI MUDA SASA WAKUWAFUNDISHA ELIMU YA AFYA YA UZAZI VIJANA BALEHE ILI KUPUNGUZA MAAMBUKIZI YA VVU

Tanzania Kids Time
Last updated: 2024/01/29 at 2:30 PM
By Tanzania Kids Time 4 Min Read
Share
SHARE

 

Nchini Tanzania umri wa balehe ni kipindi
kinachoambatana na hatari zaidi kwa wasichana, hasa kwa wale waishio katika makao
ya kulelea watoto wenye ulemavu na mazingira magumu, jambo linaloonyesha
umuhimu wa kuongeza na kuendeleza miitikio ya kuimarisha uelimishaji wa vijana
balehe kuhusu afya ya uzazi, usawa wa kijinsia, haki na maendeleo yao.

Ili kuisaidia Serikali katika kuelimisha kundi hili
lililopo kwenye hatari zaidi, vyama vya kiraia, jamii, wazazi, walezi, viongozi
wa dini, viongozi wa kimila, wasichana na wavulana balehe wenyewe wanapaswa
kushiriki kikamilifu kila mmoja kwa sehemu yake, ili kukabiliana na changamoto zinazo
wazunguka vijana hawa.

Mkoani Mbeya, Shirika la Tumaini Community Services
linatekeleza mradi wa ‘Dreams’ yaani ‘Ndoto’ katika Halmashauri ya Mbeya mjini,
Kyela na Mbarali mkoani Mbeya kwa ufadhili wa mfuko wa rais wa Marekani wa
harakati za kupambamba na UKIMWI, PEPFAR kanda ya Tanzania, lengo likiwa
kuwawezesha vijana balehe elimu ya afya ya uzazi, elimu ya kujitambua na elimu
ya kiuchumi ili kupunguza maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI, ambapo mpaka sasa zaidi ya vijana elfu 30 wamefikiwa na mradi huo kwa Wilaya hizo tatu.

Tatu
Mwambungu wa wilayani Kyela ni mnufaika wa mradi wa Dreams unaotekelezwa mkoani
Mbeya na shirika lisilo la kiserikali la Tumaini Community Services anaeleza
sababu anazofikiri kuwa ni sababu zinazowaweka matatizoni vijana balehe akisema
ni kutokana na kwamba wanakuwa hawana elimu sahihi ya afya ya uzazi akisema
kwamba wanafika umri wa kubalehe lakini, “tunakuwa hatujui kutokana na
jamii yetu wanaficha au wzazi wanaficha vile vitu ambavyo binti anatakiwa
kuvijua akishakua amebalehe.” 

 Tatu
Mwambungu yeye ameema sababu ni ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi, Vaileth
Bukuku yeye ni  mkazi wa Mbeya mjini naye anaeleza kuwa elimu ya afya
ya uzazi ina umuhimu mkubwa kwa vijana balehe n ani elimu ambayo
inatakiwa, “ipewe kipaumbele sana.” 

“Wengine
wanakatisha masomo kwa sababu ya kuzaa. Yaani ingekuwa ni elimu kubwa
ningefurahi sana ingekuwa ni elimu kubwa ambayo ingetolewa sana hususani
kuanzia darasa la 7 au la 6 kwenda juu mpaka vyuo huku juu inatakiwa iwe elimu
ambayo ni namba moja.” Anasisitiza Vaileth.  

Dkt. Steward Kilumile ni Mganga mfawidhi wa kituo cha
afya Miyombweni kilichopo Wilaya ya Mbarari anasema elimu kuhusu afya ya uzazi
inayotolewa kwa vijana anaona inaleta mabadiliko. Akisema, “kupitia mradi
kama huu wa dreams kwa kuwa wanapata elimu kwenye vikundi inazidi kuwapa vijana
upeo dhidi ya mazingirea hatarishi.” 

Jonathan Mwashilindi ni Mkurungezi wa shirika hilo la
Tumaini anasema wasichana wenye umri mdogo kutokana na kukosa muongozo mzuri
ndipo wanajikuta wanapata ujauzito wakiwa bado watoto wadogo na hawajui hao
watoto watakaozaliwa watawatunza kwa namna gani. Kwa msingi huo anatoa wito kwa
kila mtu katika jamii kushiriki katika kusaidia “ili hawa mabinti ndoto
zao waweze kziishi baadaye.” 

Mfuko wa rais wa Marekani wa harakati za kupambamba
na UKIMWI, PEPFAR kanda ya Tanzania umekuwa ukisaidia serikali ya Tanzania kuboresha
sekta ya afya kwa ujumla wake hasa katika kupambambana katika kupunguza
maambukizi ya vvu nautoaji wa elimu ya afya ya uzazi kwa vijana balehe,
jitihada hizo zimeendelea kujidhihilisha kupitia miradi mbalimbali inayo husu
afya.

 Na, John Kabambala.

You Might Also Like

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi

Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili

Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania

KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.

UWEZO TANZANIA YARATIBU KIKAO CHA MIKAKATI YA KUWASHIRIKISHA WAZAZI UELIMISHAJI VIJANA STADI ZA MAISHA.

Tanzania Kids Time May 5, 2022
Share this Article
Facebook Twitter Email Print
Previous Article HALI ILIVYO JUU YA VITENDO VYA UKATILI DHIDI YA WATOTO WAKIKE MKOA WA MOROGORO.
Next Article HISTORIA YA VAILETH BUKUKU MKAAZI WA MBEYA MJINI.
Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

Facebook Like
Twitter Follow
Youtube Subscribe
Telegram Follow
- Advertisement -
Ad image

Latest News

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
//

Tanzania Kids Time: A platform spotlighting children’s and women’s issues in Tanzania, focusing on education, health, and environmental conservation.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

© 2023 Tanzania Kids Time. Powered by Digital Media Innovation Program. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?