nchini Tanzania inaonesha watu wanaoishi na VVU hadi kufikia mwezi
Disemba mwaka 2020 watu wazima wenye umri wa kuanzia miaka 15 na zazidi ni
1,600,000, Wanawake 1,000,000, Wanaume 600,000 na Watoto chini ya miaka 15
ilikuwa 100,000 Jumla watu wazima na
watoto ni 1,700,000.
Maambukizi
mapya ya VVU kwa kipindi hicho
Watu wazima Zaidi ya miaka 15 wailikuwa 58,000 Wanawake 37,000, Wanaume 21,000
na Watoto chini ya miaka 15 walikuwa 10,000 Jumla watu wazima na watoto 68,000.
Vifo vitokanavyo na UKIMWI kwa mwaka 2020 Watu wazima Zaidi ya
miaka 15 vilikuwa 24,000 Wanaume 11,000 elfu, wanawake 13,000 elfu na Watoto
chini ya miaka 15 ilikuwa elfu 8,000, Jumla
ya vifo watu wazima na watoto ilikuwa 32,000 elfu.
Tukiugeukia
Mkoa wa Mbeya, Takwimu
zinaonesha kwamba Mkoa huo upokwenye nafasi ya tatu kwa ongezeko la maambukizi
ya virusi vya UKIMWI hasa kwa vijana walio katika umri wa rika balehe kwa
asilimia 9.3%, Mkoa wa Njombe ukiwa
nafasi ya kwanza kwa kuwa na maambukizi ya asilimia 11.4% ukifuatiwa na Mkoa wa Iringa kwa kuwa na maambukizi ya asimia
11.3%, Takwimu hizo ni kwa mujibu wa
Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) mwaka 2020.
Shirika la Tumaini
Community Services lenye makao yake makuu Mkoani Mbeya baada ya kuona ongezeko
la maambuki ya virusi vya UKIMWI kwa vijana balehe walio kati ya umri wa miaka
kumi natano hadi ishirini na nne yanashamiri, walianzisha mradi wakuwawezesha
vijana kupata elimu ya afya ya uzazi, elimu ya upimaji wa vvu, elimu ya
kujitambua na elimu ya uchumi.
Mradi huo
unajulikana kama DREAMS unatekelezwa Mkoani Mbeya kwa Wilaya tatu ambazo ni
Mbeya mjini, Kyela na Mbarali kwa ufadhili wa mfuko wa rais wa marekani wa
harakati za kupambana na UKIMWI, PEPFAR kanda ya Tanzania, ambao unalenga
kupunguza maambukizi ya virusi vya UKIMWI kwa vijana kwa kuwapatia elimu ya
kujikinga na maambukizi ya vvu, elimu ya kujitambua, na elimu ya kiuchumi.
Katika halmashauri
ya jiji la Mbeya nimezungumza na kijana mwenye umri wa miaka ishirini na mbili sasa
mama wa watoto wawili anaeishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi, kwa ridhaa
yake amerusuhu jinalake halisi litumike kwa matumizi ya kuwaelimisha vijana
kuhusu hali ya maambukizi ya vvu ambae ni Vaileth Bukuku.
Vaileth Bukuku ni mzaliwa wa Mbeya mjini, akiwa na
umri wa miaka nane (8) alipata maambukizi ya virusi vya Ukimwi kwa kufanyiwa
ukatili wa kubakwa akiwa nyumbani kwao Mkoani Mbeya, “Nakumbuka ilikuwa sikukuu ya pasaka dada yangu aliniacha nyumbani
nikiwa na njaa akaenda kwenye disko maana siku hiyo alikuja kaka mmoja nyumbani
ambae alikuwa na mazoea na dada yangu alipofika akaniuliza Vaileth umekula?
Nikamwambia hapana sijala akaniambia njoo uchukue pesa ukanunu mchele uje
upike, akanipatia shiringi elfu moja nikaenda dukani kununua mchele.
Badae alirudi tena huyo kaka
akaniuliza unatamani kunywa soda? Nikamjibu ndio natamani akaniambia twende
ukachukue soda, yule kaka hakunipeleka dukani akanipeleka chooni tulipofika
chooni alinibaka nikaumia sana yeye akaondoka nikajikokota kutoka chooni nikashindwa
hata kuingia ndani, dada alipokuja usiku sana akanikuta mlangoni akanibeba
nikamuelezea jinsi ilivyo kuwa akachemsha maji yamoto akanikanda akanipatia na
panado akanimbia usimwambie mtu yeyote, Amesema.
Aidha Vaileth alipofikisha miezi mitatu
baadae alianza kuumwa mara kwa mara vidonda vikaanza kumtoka akashindwa hata
kuudhulia masomo shuleni, Vaileth anasema “siku
moja alikuja jirani yetu nyumbani akaniuliza mbona sikuhizi hujikucheza na
watoto wenzako nyumbani na sikia hata shuleni huendi unatatizo gani,
sikumwambia kesho yake akarudi tena ikabidi nimwambie ukweli kuwa mimi nina
umwa akanichukuwa akanipeleka hospitali tulipofika daktari akamwambia yule mama
aenda polisi akachukue pf3 maana anaonekena huyu binti kunakitendo alifanyiwa
mbali na magonjwa ya zinaa anamaambukizi ya virusi vya ukimwi ”.
Mwaka 2019
mradi wa Dreams ukamfikia Vaileth Bukuku kwa sababu alikuwa ndani ya vigezo
mradi ulikuwa ukivitaka kwa vijana waliokuwa katika mazingira hatarishi ya
kupata maambukizi ya virusi vya Ukimwi, na walio wahi kubeba ujauzito wakiwa
katika umri mdogo wanaoishi kwenye Wilaya ambazo zimelengwa kutekelezwa mradi,
ambapo huduma ya upimaji ili kujua hali zao za maambukizi ya virusi vya Ukimwi ilifanyika
kisha kuwa wanufaika wa mradi huo.
Hata hivyo
wataalamu kutoka shirika la Tumaini Community Services walimshauri Vaileth kuwa mfusi mzuri wa matumizi ya
dawa za kufubaza virusi vya Ukimwi na kuendelea kujilinda yeye mwenyewe na
kuwalinda wengine ilikutoendelea kuchochea maambukizi mapya kwa jamii, hasa kwa
vijana balehe.
Anashukuru
mradi wa Dreams kupitia shirika la Tumaini
Community Services kwa kumpeleka chuo cha ufundi VETA kujifunza ufundi wa
kushona na matumizi ya kompyuta ambao baada ya kuhitimu walikabidhiwa vyeleani
kila binti mnufaika wa mradi huo alie somea masuala ya ushonaji, na sasa
wamejiajili wenyewe kwa kufungua ofisi ya kushona nguo na kujipatia kipato, wakati
huo wakiwa niwaelimishaji wa vijana kuhusu kujikinga na maambukizi ya vvu
ikiwemo kutumia kondom wakati wa kufanya ngono.
Malengo ya
Vaileth yalikuwa kusoma na kuwa muhandisi wa kompyuta, lakini sasa anaona
ameshindwa kuyatimiza kwa sababu tiyari ameshapata watoto wawili na yeye ndio
mzazi pekee anaewahudumia pasipo kuona usaidizi kutoka kwa wazazi wenzie wa
watoto hao, hivyo basi anasema nguvu nyingi amewekeza kwa watoto wake
kuwaandalia mazingira mazuri ya kuja kusoma ili baadae watimize ndoto zao.
Ushauri wake
kwa vijana ambao tiyari wanaishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi wafuati
ushauri wa wataalamu wa afya ikiwemo kuzingatia muda wa matumizi sahihin ya
dawa za kufubaza virusi vya ukimwi, wajilinde na wawalinde wengine wasisambaze
virusi vya Ukimwi kwa makusudi kwa wale ambao hawajapima kujua hali zao za
kiafya wajitokeze wakapime kujua hali zao ilikuishi kwa Amani na furaha,
ilikama hawana maambukizi waendelee kuwa waamifu na wale ambao watagundulika
kuwa na maambukizi ya vvu waanze kliniki mapema.
Na. John Kabambala.