Wanawake wanaonyonyesha watoto, wameahidi kuzingatia mlo wa makundi matano ya Chakula ili kujenga na kulinda Afya ya Mtoto aliye chini ya umri wa miaka Sita, katika ukuaji wa akili na Mwili wake.
Hamad Rashid, alihudhuria sherehe za maadhimisho ya Wiki ya unyonyeshaji Mkoa wa Morogoro yaliyofanyika katika viwanja vya Kata ya Mkambalani Kijiji cha Mkambalani Manispaa ya Morogoro na kuandaa Makala ifuatayo.
Fadhila Yusufu ni mmoja wa wanawake waliohudhuria maadhimisho ya wiki ya unyonyeshaji mtoto maziwa ya mama na ana mtoto mwenye umri wa miezi sita. Mama huyu ni mkazi wa kijiji cha Mkambalani, hapo hapo mkoani Morogoro, alisema unyonyeshaji kwake ndio kipaumbele kikubwa kwa mtoto wake.
“sasa hivi tulivyotoka hapa inamaana tutaongeza juhudi za unyonyeshaji kwanza Dakika 45 mpaka dakika 60.” Na mimi uji lishe huwa natengeneza mwenyewe ukiwa na makundi manne ya chakula halafu Tunda kama kundi la Tano natumia baada ya kumalisha kupika uji’’ alisema Fadhila Yusufu
Mtoa huduma za afya kitengo cha Mama na Mtoto katika Zahanati ya Kata ya Mkambalani Rebeka Wami alithibitisha wanawake kuwa na mwamko wa kunyonyesha watoto wao kwa mujibu wa malekezo ya wataalamu wa afya.
“Katika siku yetu hii ya unyonyeshaji, tumeweza kupata uzoefu wa kipekee ambao tumeona akina mama wengi wanahamasika na unyonyeshaji wa maziwa pekee kwa mtoto chini ya miezi sita. Na ukanda huu akina mama wengi wanaonekana wamepata elimu na elimu hii imeweza kuwasaidia kunyonyesha watoto wao na kuondoa hali ya utapiamlo.” Alieleza mtoa huduma ya afya, Rebeka Wami.
RAJABU SHABANI Baba wa Familia katika Kijiji cha Mkambalani alisema katika kipindi cha mke wake kunyonyesha huwa anawajibika ipasavyo kumhamasiha.Rajabu alisema,
“mimi huwa namsaidia kazi mke wangu akiwa ananyonyesha labda naosha vyombo au kufua yeye akiwa anamnyonyesha Mtoto n ahata yeye akiwa anakazi nambeba Mtoto, nawahamasisha akina Baba wengine kuwasaidia wake zao shughuli ndogo ndoto pindi wanaponyonyesha”
Akizungumzia malengo ya wiki ya unyonyeshaji Afisa Lishe Manispaa ya Morogoro Bi ESTHER CHACHA alieleza pia kwamba “Mtoto anaponyonya maziwa ya Mama kwa muda wa miezi sita bila kula na kunywa chochote inamsaidia katika kukua akiwa na akili nzuri, kumpa kinga ya asilia ya Mwili na niwaambie maziwa ya Mama yanakila aina ya virutubisho anavyopashwa kupewa Mtoto”
Bi, Esther aliongeza kuwa “ni muhimu sana Mtoto kunyonyeshwa ndani ya saa moja baada ya kuzaliwa kwani yale maziwa huwa ndio yanakinga nyingi kwa Mtoto na husaidia kukata Damu kwa Mama aliyejifunua”
Sherehe za maadhimisho ya Wiki ya Unyonyeshaji kimkoa zimeandaliwa Serikali la Mkoa wa Morogoro kwa kushirikiana na Shirika la save the children kupitia mradi wake wa USAID LISHE ENDELEVU kwa hisani ya watu wa Marekani.
Aidha chanjo ya Vitamin A na dawa za minyoo zilitolewa kwa watoto wa miezi sita hadi miaka mitano katika maadhimisho hayo ilihali burudani ya muziki wa mwambao umetolewa na Mtumbuizaji MARIAM MAMBO kupambiza sherehe hizo.
Na Hamad Rashid.