By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
Tanzania Kids Time
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Mazingira
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Wasiliana Nasi
Reading: JINSI YA KUBORESHA MTAALA WA ELIMU YA AWALI
Share
Notification Show More
Latest News
Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
TANZANIA WILL HOST CIGOFA4 TO FIND CONCRETE SOLUTIONS FOR YOUTH LAND QUESTIONS
Editor's Pick
Aa
Aa
Tanzania Kids Time
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
  • Contact
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Tanzania Kids Time > Blog > Elimu > JINSI YA KUBORESHA MTAALA WA ELIMU YA AWALI
ElimuUncategorized

JINSI YA KUBORESHA MTAALA WA ELIMU YA AWALI

Tanzania Kids Time
Last updated: 2024/01/29 at 2:30 PM
By Tanzania Kids Time 7 Min Read
Share
SHARE

TATIZO NI NINI?


Tatizo ni mtaala wa Elimu ya Awali kutokidhi mahitaji ya watoto ya kujengewa umahiri wa kujua kusoma, kuhesabu, kuandika, na kushindwa kushirikisha wananchi na walimu wa darasa la Awali ipasavyo wakati wa uandaaji na uboresjaji wa mtaala huo.

Kwamujibu wa mtaala wa Elimu ya Awali unaonesha kabla ya mwaka 2005, Uliweka msisitizo wa kufundisha maudhui ya masomo, Mwaka 2005, Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo, iliuboresha mtaala huo kwa kuweka msisitizo zaidi katika ujenzi wa umahiri wa watoto badala ya maudhui.

Pamoja na maboresho hayo yote bado watekelezaji waliendelea kusisitiza zaidi maudhui kuliko ujenzi wa umahiri kwa watoto hasa katika shule za Serikali kama mtaala ulivyokuwa ukiwata.

Mwaka 2016 yalifanyika maboresho mengine ya mtaala huo yakizingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 2014, pamoja na matokeo mbalimbali ya tafiti na mapendekezo kutoka kwa wadau wa elimu yanaonesha kwamba, mtoto akijenga msingi imara wa kujifunza katika Elimu ya Awali atakuwa tayari kuanza darasa la I na kuendelea vizuri katika ngazi zingine za elimu.

Mwaka 2021, Wizara ya Eilimu, ilianza tena mchakato wa kuboresha mitaala ya ngazi mbali mbali ya Elimu ukiwemo mtaala wa Elimu ya Awali, swali nije, wananchi wanashirikishwa vya kutosha?
Mwalimu Gipson Mosi anasema wananchi na walimu hasa wa elimu ya Awali hawashirikishwi ipasavyo.

“Serikali inafanya maboresho ya mtaala lakini inashindwa kuusimamia” huyo ni Nasha Sota siojina lake halisi mkazi wa Bigwa Manispaa ya Morogoro, amesema.

Abdul Dachi mkazi wa Tungi Manispaa ya Morogoro anasema mtaala wa Elimu ya Awali haujulikani ipasavyo na hata kwenye vikao vya mtaa,vijiji hata ngazi ya kata hauzungumziwi.


CHANZO CHA TATIZO NI NINI?

Wananchi hawajashirikishwa vyakutosha, Mfano: “Tangu mwaka 2021 Serikali imeanza kukusanya maoni ya uboreshaji wa mitaala ukiwemo huu wa darasa la Awali je, watanzania wangapi hadi sasa wanafahamu kwamba wanatakiwa kutoa maoni yao juu ya uboreshaji wa mtaala kama huu ? utakuta wachache ndio wanataarifa hii” Amesema Mwl.Gipson Mosi kutoka Manispaa ya Morogoro.

Wananchi na walimu wa darasa la awali tena kutoka mjini na vijijini nimuhimu kuwajumuisha katika kuchukuwa maoni ya uborehaji wa mtaala huu kwa ukamilifu, Nawakati wa kufanya maboresho ya mtaala huo hawakuweka kipaumbele kutumia vyombo vya habari kuwatangazia wananchi umuhimu na wajibu wao kushiriki kutoa maoni yao juu ya uboreshaji wa mtaala huo.

Aidha Mwl.Mosi anasema “Leo hii wakikusanywa watanzania miamoja (100) lisiwemo kundi la waratibu elimu, walimu au maafisa elimu yawezekana watano tu kati yao, ndio wanaweza kufahamu kwamba darasa la awali lina mtaala wake, Zaidi ya hapo wananchi wengi hawafahamu na matokeo yake mtoto anafundishwa jambo lingine shuleni akirudi nyumbani anasisitiziwa jambo lingine”.

Kwamujibu wa Muhtasari wa Ripoti ya Elimu tunayo itaka ya Mwaka 2021 kutoka Shirika la Haki Elimu Tanzania, inaonesha Vitabu vya kiada vya shule haviendani na mtaala unaolenga kukuza umahiri wa watoto. Na mfumo wa sasa wa upimaji wa umahiri wa watoto unahimiza kujifunza kwa kukariri na ushindani usio na tija kati ya watoto, huku ukiwaacha nyuma watoto wengine wenye mahitaji maalum.

Nasha Sota ambae ni mwalimu na muajiliwa wa serikali anasema “Tatizo lililopo kwa muajiliwa wa Serikali kama Mimi siwezi kuhoji sana kwa mwajili wangu kuhusu mtaala hata mpango kazi wake, kwasababu unakuta hata vitendea kazi vyakutosha hakuna kamavile midori ya namba, herufi, wanyama, mipira nk, ambavyo hivi ndivyo vinawasaidia watoto kuelewa kwa haraka zaidi”.

“Matokeo yake tatizo la baadhi ya watoto wanamaliza mwaka mzima kwenye darasa la Awali pasipo kujua kusoma irabu, kuziandika na kuhesabu, hatimae wakianza darasa la kwanza hawatakuwa imara nahata kujiamini jambo linalo chochea kuwepo kwa bora Elimu badala ya elimu bora kwa kila mtanzania” bi, Sota amesema.

Kitengo cha Elimu kutoka Shirika la Kimataifa la kuhudumia watoto Duniani Unicef Tanzania kinaonesha upatikanaji wa elimu ya awali ni mdogo sana, na ubora duni unaofifisha matarajio ya watoto ya mustakabali wao wenye tija kwa siku zijazo.

Uwiano wa wanafunzi kwa mwalimu wanaohitimu katika ngazi ya shule ya Awali ni 131:1, Uwiano huu ni 169:1 katika shule ya awali za umma ikilinganishwa na 24:1 katika shule za kibinafsi, Watoto wengi hasa wa maeneo ya vijijini wanaingia shule za msingi wakiwa hawana maandalizi ya kutosha na ubora duni wa elimu ya awali.

NINI KIFANYIKE?

Serikali ishirkiane na shule binafisi katika uwekezaji wa elimu kwa vitendo kwa watoto kama vile kuzalisha zaidi vitendea kazi kwa maana ya zana muhimu ambazo zitatumika Zaidi kuwafundishia na kuwajengea umahiri watoto, sambamba na kupunguza muda wa maandalio, huyo ni mwalimu wa darasa la Awali Sara Mpiga kutoka shule ya Baptist iliopo Manispaa ya Morogoro.

Bi, Maria Sabasi ni mmiliki wa kituo cha kulelea watoto mchana kijulikanacho kwa jina la Mary Day Care Cantre kilichopo Manispaa ya Morogoro, maoni yake juu ya mtaala wa Elimu ya Awali ujao anatamani kuona Serikali imeweka mpango wa kutoa ruzuku ya vitendea kazi/nyenzo za kufundushia kwenye vituo vya kulelea watoto mchana na shule zilizo na darasa la Awali.

Maoni ya Nd. Abdul Dachi anasema ili kuboresha mtaala wa Elimu ya Awali, na kupata maoni kutoka kwa wananchi na wadau wa Elimu hiyo kuna haja yakusanywe kutoka mjini na vijijini tena kwa walengwa ambao ni walimu na wamiliki wa vituo vya Awali, na Serikali yaweza kuufanya mchakato huu kuwa agenda itakayo zungumziwa kupitia vikao vya ngazi ya mtaa, vijiji na kata.

Mwl. Gipson Mosi yeye anaishauri Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na Taasisi ya Elimu Tanzania ambazo ndio zenyedhamana ya uandaaji wa mitaala yote, zitumie vyombo vya habari kikamirifu, kuufahamisha umma kuhusu utoaji maoni ya uboreshaji wa mtaala wa Elimu ya Awali.

Na, John Kabambala – Morogoro.

You Might Also Like

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi

Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili

Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania

KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.

ENERGY AND NEO-COLONIALISM IN AFRICA, NO ANSWERS?

Tanzania Kids Time September 25, 2022
Share this Article
Facebook Twitter Email Print
Previous Article ISSA IBRAHIM MGONJWA WA MWISHO WA POLIO TANZANIA
Next Article TATIZO LA KUOZA MENO WATOTO
Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

Facebook Like
Twitter Follow
Youtube Subscribe
Telegram Follow
- Advertisement -
Ad image

Latest News

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
//

Tanzania Kids Time: A platform spotlighting children’s and women’s issues in Tanzania, focusing on education, health, and environmental conservation.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

© 2023 Tanzania Kids Time. Powered by Digital Media Innovation Program. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?