By using this site, you agree to the Privacy Policy and Terms of Use.
Accept
Tanzania Kids Time
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Mazingira
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Wasiliana Nasi
Reading: TATIZO LA KUOZA MENO WATOTO
Share
Notification Show More
Latest News
Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
TANZANIA WILL HOST CIGOFA4 TO FIND CONCRETE SOLUTIONS FOR YOUTH LAND QUESTIONS
Editor's Pick
Aa
Aa
Tanzania Kids Time
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Home
  • Afya
  • Elimu
  • Haki Za Watoto
  • Uchambuzi na Takwimu
  • Mazingira na Mabadiliko ya Tabianchi
  • Contact
Follow US
  • Advertise
© 2022 Foxiz News Network. Ruby Design Company. All Rights Reserved.
Tanzania Kids Time > Blog > Afya > TATIZO LA KUOZA MENO WATOTO
AfyaUncategorized

TATIZO LA KUOZA MENO WATOTO

Tanzania Kids Time
Last updated: 2024/01/29 at 2:30 PM
By Tanzania Kids Time 7 Min Read
Share
SHARE

Pembezoni mwa safu za milima uluguru nikati ya mitaa yenye utulivu isio kuwa na kelele zaidi yakusikia sauti za ndege na wadudu, sio kwamba kuna ulinzi wa hali ya juu Zaidi kama ule wa “CHAMWINO AU MAGOGONI”, la hasha, hapa ni bong’ola mojawapo ya mtaa katika Manispaa ya Morogoro alipozaliwa Ashera, wanaoishi mtaa huu niwenye kipatoa cha uhakika kwa asilimia 70% nakuendelea, hivyo pesa kwao sio tatizo sana.


Miongoni mwa sifa kubwa za mtaa huu, hakuna daladala zinazokuja kuchukua au kushusha abiria katika eneo hili, isipokuwa ni usafiri binafsi au magari ya taasisi na Serikali pekee ndio hukatiza maeneo haya, hali ya hewa ni joto kiasi na baridi Zaidi hasa nyakati za usiku, hii inatokana na utunzaji mzuri wa mazingira yenye miti asilia na iliopandwa kwa mpangilio.

Akiwa na umri wa miezi 18 tu, Ashera mtoto wakwanza kwenye familia yao, Mama yake anaeitwa Alvera anaanza kumpatia pipi na chokoleti mdomoni mwake, ladha alioihisi siku hiyo kwenye ulimi wake hakuwahi kuipata kabla tangu kuzaliwakwake.

Makala hii imejumuisha watu wanne ambao ni Mtoto Ashera alieoza jino, Mzazi wake jina Alvera Morie, Daktari wa kinywa na meno na Muuzaji wa duka la dawa muhimu. Ashera ndiye muhusika mkuu katika Makala hii.

NJOO NAMI ILI UJUE HALI YA TATIZO ILIVYO.
Kwanza kabisa, nini maana ya tatizo la kuoza meno watoto? Daktari Shukrani Mapunda kutoka Baraka Poly Clinic kituo kinachotoa huduma za afya ikiwemo ya kinywa na meno, kilichopo Manispaa ya Morogoro anafafanua. “Ni hali ya sehemu ya juu na ndani ya jino kutoboka, na watoto wadogo ndio waathirika Zaidi wa tatizo hili wakiwa katika umri mdogo”.

Kwa mujibu wa takwimu za kituo hicho, Daktari. Mapunda anasema, kwa Manispaa ya Morogoro kila mwezi hupokea watoto Zaidi ya kumi 17 wenye matatizo ya kuoza/kutoboka meno, ambao huitaji kuzibwa au kung’oa kabisa.

“Nilianza kutumia vijiti kuchokonoa jino, baadae lika anza kuuma nikawa ninalia nikashindwa hata kula chakula,” Ashera anasema.

Alvera Morie mkazi wa Bong’ola Manisapaa ya Morogoro, alianza kusikia harufu mbaya inayo nuka, wakati mtoto wake anapo ongea au kufumbua mdomo ambae ni Ashera.
Mary Silvester yeye ni muuzaji wa dawa muhimu, kutokea Kihonda Morogoro anasema maranyingi anauza dawa za mswaki aina ya Whitedent kwa sababu wateja wengi wanakuwa wameshauriwa na wataalamu wa afya.

CHANZO CHA TATIZO LA KUOZA MENO WATOTO NI NINI?
Kwa mujibu wa kitabu cha mtindo wa maisha kilicho andaliwa na Wizara ya afya kushirikiana na Shirikisho la vyama vya magonjwa yasiyo ambukiza Tanzania (TANCDA) kinaonesha asilimia 60-90 ya watoto wote walio na umri wa kwenda shule duniani kote, wana ugonjwa wa meno kutoboka. Nchini Tanzania, kwa Watoto wenye umri kati ya miaka 4-6 mtoto mmoja kati ya watoto watatu anajino lililotoboka/kuoza.

AINA GANI YA VYAKULA HUSABABISHA TATIZO HILI?
Ulaji wa mara kwa mara vyakula vyenye sukari Zaidi kama vile, Pipi, Chokoleti, Bisukti, Visheti, Ubuyu wenye sukari, Kashata, Keki, Isikrimu na Juisi za viwandani.

DAWA ZINASABABISHA KUOZA MENO WATOTO?
Ndio, Utumiaji holela wa dawa za maji zinazo tumika kwa watoto, hususani za kutibu kikoozi na kifua zimewekwa sukari ili kushawishi watoto wapende kuzinywa, nimojawapo ya visababishi vya kuoza/kutoboka meno kwa watoto.

“Nilikuwa na mpatia vitu vitamu kamavile pipi na chokoleti wakati anapolia ikiwa mojawapo ya mbinu ya kumnyamazisha” bi, Alvera, hayo ndio yalikuwa mawazo ya mzazi na walezi wa Ashera, taratiiiibu mtoto akaizoea radha ile nakujua kwamba nimoja kati ya haki na sehemu ya mlo wake wa kila siku.

DALILI ZA KUOZA JINO ZILIONEKANA LINI KWA ASHERA?
Mwaka 2022 Ashera ana miaka sita 6 sasa, anaanza kuchokonoa meno kwa vijiti pamoja na harufu mbaya kutoka mdomoni mwake, hatimae shavu la kushoto likavimba na kuanza kutoa usaa kwenye fizi ya jino la juu kushoto, wakati wotenikulia na kuita mama jino linauma hatakula ikashindikana.

NINI HUTOKEA JINO LIKIOZA NA KUTOTIBIWA MAPEMA?
-Usaha kusambaa usoni, Shingoni, Kifuani na hata kwenye mapafu, Maambukizi kuingia kwenye mifupa ya taya, Mfumo wa damu na Ubongo, Kupungua kwa ubora wa maisha, kuathiri mahudhurio na ufanisi masomoni nanyingine nyingi.

Bi, Alvera anasema, “Nilimchukua mtoto kwendanae kwa Daktari wa kinywa na meno kumuelezea historia fupi ya aina ya vyakula anavyokula hadi kipindi tatizo lilipo anza, Dr. alivyo minya fizi ya Ashera penye jino lililo oza ulitoka usaha kupitia kinywani.

Kisha akazibwa palipo toboka lakini hatua hiyo haikumsaidia kwani aliendelea kulia kwa uchungu, baada ya siku tatu nikampeleka kwa daktari wa kinywa na meno kituo cha Baraka Poly Clinic akaling’oa, ndio kupona kwa Ashera hadi sasa yuko vizuri na hakuna tena harufu mbaya mdomoni inayo toka” Alvera anasema.

NINI KIFANYIKE KUEPUSHA KUOZA MENO WATOTO?
Dr. Mapunda anasema, wazazi/walezi wanapaswa kusitisha vyakula na vinywaji vyenye sukari nyingi kwa watoto wadogo, madhala yake ni kuoza/kung’oa meno kabisa. Watoto wapelekwe kwa Daktari wa kinywa na meno kufanyiwa uchunguzi wanapofikisha miezi 9 hadi mwaka 1, kupiga mswaki marambili kwa siku, asubuhi na baada ya mlo wa usiku kwa kutumia dawa aina ya Whitedent yenye fluoride.

Ashera anawashauri watoto wenzake waache kula vituvitamu vyenye sukari nyingi, ili wasioze meno kama jino lake lilivyo oza, “Daktari aliniambia kwa sababu ulikula pipi na chokoleti ndio maana jino limeoza na tunaling’oa, ili meno yasioze usile pipi, chokoleti na visheti, sitaki tena kula vitu vitamu na ninazingatia kupiga mswaki mara mbili kwa siku” Amesema.

Mary Silvester anawashauri wazazi na walezi kuhakikisha wanapunguza kuwanunulia watoto wao vitu vitamu na badala yake waandae nyumbani, ilikudhiti tatizo hilo kwa watoto.

Alvera ambae mwanae ameng’olewa jino kwa sababu ya pipi na chokoleti alizo kuwa akimpatia mwenyewe, anasema hatarudia tena kumpatia vituhivyo, na sasa anaishauri jamii kuepuka zawadi za pipi, chokoleti, keki nk, kuwanunulia watoto kwani madhala yake amejionea mwenyewe, anashukuru Ashera amepona na anendelea na masomo yake akiwa na afya njema.

Kwa utafiti mdo nilioufanya katika Manispaa ya Morogoro unaonesha kwamba, asilimia kubwa ya watoto wanao fikishwa kwenye huduma za afya kwa tatizo la kuoza meno, wanatokea familia zenye kipato cha kati na cha juu, ambako kunauwezekano wa mzazi kumnunulia mtoto wake pipi, chokoleti, keki nk, wakati anapoviomba vitu hivyo. Wewe ndio mlinzi wa mtoto usiendelee kumpatia kila anacho kililia ili uonekane unampenda kata ilinde afya yake.

Na, John Kabambala – Morogoro.

You Might Also Like

ENERGY AND NEO-COLONIALISM IN AFRICA, NO ANSWERS?

THROUGH MZF NOW TRADITIONAL BIRTH ATTENDANCE THEY IMPROVE WOMEN’S WELL-BEING FOR SAFE DELIVERY

TOWARDS TEN YEARS OF MILELE ZANZIBAR FOUNDATION, READ THE ACHIEVEMENTS OF THE SHEHIA PROJECT

MABADILIKO YA HALI YA HEWA NITISHIO LINALOWAKABILI WANAWAKE WAJAWAZITO NA WATOTO.

MTI WA MATUMAINI WA ZINDULIWA ARUSHA: UNICEF

Tanzania Kids Time October 4, 2022
Share this Article
Facebook Twitter Email Print
Previous Article JINSI YA KUBORESHA MTAALA WA ELIMU YA AWALI
Next Article MAZUNGUMZO NA MABINTI WALIOJIFUNGUA NA KURUDI SHULENI
Leave a comment

Leave a Reply Cancel reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Stay Connected

Facebook Like
Twitter Follow
Youtube Subscribe
Telegram Follow
- Advertisement -
Ad image

Latest News

Mapendekezo ya Mradi wa Sauti zetu ni Muhimu kwa Mkakati wa Elimu Jumuishi
Elimu Haki Za Watoto
Mafanikio ya Shirika la SAWA Kuwezesha Wazazi Kuziishi Stadi za Maisha na Maadili
Elimu
Sababu ya Mradi wa ALiVE Kufanikiwa Kutengeneza Vinara Zaidi ya 300 Tanzania
Elimu Haki Za Watoto
KONGANI YA ELIMU YA MTANDAO WA ELIMU WA KIKANDA – RELI AFRIKA YAONGOZA MAADHIMISHO YA SIKU YA WALIMU DUNIANI.
Elimu
//

Tanzania Kids Time: A platform spotlighting children’s and women’s issues in Tanzania, focusing on education, health, and environmental conservation.

Sign Up for Our Newsletter

Subscribe to our newsletter to get our newest articles instantly!

© 2023 Tanzania Kids Time. Powered by Digital Media Innovation Program. All Rights Reserved.

Join Us!

Subscribe to our newsletter and never miss our latest news, podcasts etc..

Zero spam, Unsubscribe at any time.

Removed from reading list

Undo
Welcome Back!

Sign in to your account

Lost your password?