“Kubeba ujauzito mtoto wakike ukiwa bado mwanafunzi ilikuwa nikama kitendo cha aibu kwa familia, jamii na hata shule husika, mbaya Zaidi hata ukijifungua hapakuwa na ruhusa ya kurejea Shuleni kuendelea na masomo”.
Huyo ni Profesa , nilipo zungumza nae kuhusu ruhusa ya wanafunzi wakike waliojifungua kurejea shuleni kuendelea na masomo katika mfumo rasimi, na haya ni machache tu, kati ya mengi utakayo jifunza kupitia Makala hii.
TATIZO NI NINI?
Ikiwa zimebaki siku thelathini na sita tu, (36) ilikutimia mwaka mmoja tangu Waraka wa Elimu No.02 wa mwaka 2021 utangazwe kuhusu urejeshwaji shuleni wanafunzi waliokatiza masomo katika Elimu ya Msingi na Sekondari kwa sababu mbali mbali, ikiwemo kubeba ujauzito je, ni hatuazipi zimefikiwa hadi sasa? Nimefuatilia utekelezaji wa Waraka huu kwenye baadhi ya Shule za Sekondari katika Manispaa ya Morogoro.
“Tatizo ni Utayari wa wanafunzi waliobeba ujauzito na kujifungua kuruhusiwa kurejea Shuleni kuendelea na masomo katika mfumo rasimi, inaonesha hawana utayari miongoni mwao”.
Waraka wa Elimu No.02 wa mwaka 2021, Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia ilitoa maelekezo ya utekelezaji wa Waraka huo, kuanzia tarehe 24 November, 2021.
Miongoni mwa vipengere vya utekelezaji mojawapo ni kipengere cha tatu kinacho sema Wakuu wa Shule/Walimu wakuu wahakikishe mwanafunzi alie katiza masomo anarejea mwanzoni mwa mwaka wa masomo katika darasa alilokuwa anasoma. Aidha Waraka unawataja Viongozi wa Elimu katika ngazi zote wafuatilie na kutahimini utekelezaji wa Waraka huu.
CHANZO CHA TATIZO HILI NI NINI?
Tangu kipindi cha uongozi wa awamu ya Kwanza, awamu ya Pili, awamu ya Tatu, awamu ya Nne na awamu ya Tano, kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi hapakuwa na ruhusa yeyote, dhidi wanafunzi wakike walio wahi kubeba ujauzito kisha kujifungua na kurejea shuleni kuendelea na masomo ndani ya mfumo rasimi.
Prof. Aurelia Kamzora yeye ni mkufunzi katika chuo kuu cha Mzumbe kilichopo Mkoani Morogoro, anasema zamani wakati wanasoma wao hapakuwa na nafasi ya kurejea shuleni kuendelea na masomo, baada ya kujifungua. “Kile kipindi kuanzia awamu ya kwanza hadi awamu ya tano nafasi hiyo haikuwepo, na wanafunzi wakike tulisoma huku tukijiuliza endapo utabeba ujauzito Shule kwako basi, mbali na kuifedhehesha familia na Shule yako.
Neema hii imejitokeza kwenye kipindi cha uongozi wa Awamu ya sita unaosimamiwa na Mh. Rais Samia Suluhu, hii nimojawapo ya njia ya kumkombo mtoto wa kike, kutoka kwenye ugandamizwaji na hata ukatili wa kijinsia. Tena njia hii nimkombozi katika maisha msichana huyo ikiwa nipamoja na kujiamini, kujisimamia na kuamua mambo yake mwenyewe, tangu nchi hii ipate uhuru jambo hilo lilikuwa mwiko. Watoto wakike wanapaswa kujitokeza na kuizingatia nafasi hiyo ili wazifikie ndoto zao”.
Kwa mujibu wa takwimu zilizo chapishwa katika tovuti ya halmashauri ya Manispaa ya Morogoro, zinaonesha kwamba halmashauri hiyo inashule 50 za Sekondari, Shule tatu kati yake ndizo nilizo pewa kibari cha kufanya mahojiano na wanafunzi wakike walio kuwa wamekatiza masomo kwa sababu ya ujazito na kurejea shuleni kuendelea na masomo. Shule hizo ni, Shule ya Wasichana Kilakala, Kayenzi Sekondari na Mwembesongo Sekondari.
Ofisi ya Mkuu wa Shule ya Sekondari Kilakala amesema hadi mwezi October 2022, wanafunzi wakike waliokuwa wamebainika kuwa na ujauzito na kukatiza masomo yao tangu mwaka 2020 ni wanafunzi watano 5. Wanafunzi watatu kati ya hao, walirudi shuleni kuomba kuendelea na masomo, ingawa waliomba uhamisho kwenda shule zingine.
Mmoja aliomba uhamisho kwenda shule ya Tabora Girls ya Mkoani Tabora, Wapili aliomba uhamisho kwenda shule ya binafsi kuendelea kidato cha tano na Watatu yeye amejiunga na chuo cha masuala ya Afya. Wanafunzi wawili walio baki hadi sasa uongozi wa shule hauna taarifa zao, kuhusu utaratibu wakuendelea na masomo.
Safari yangu haikuishia hapo, moja kwa moja nikaelekea Shule ya Sekondari Kayenzi, ambapo nakutana na Mwalimu Delphine Gervas huyu ni msimamizi mkuu katika kitengo cha malezi kwenye Shule hii ambayo ni mchanganyiko yaani Wavulana na Wasichana.
Takwimu za wanafunzi wakike waliobeba ujauzito zilizo thibitishwa na daktari kuanzia mwaka 2020, zilionesha kuna wanafu wakike watatu (3) walio kuwa na ujauzito, na mwaka 2021 wanafunzi watatu (3) waligundulika kuwa ni wajawazito.
Mwl. Delphine anasema, “mwaka 2020 tulihisi kwamba baadhi ya wanafunzi wakike shuleni hapa wana ujauzito, baada ya vipimo vya Daktari vilionesha nikweli wanafunzi watatu wanaujauzito. Mwaka 2021 pia tulipo wapima wanafunzi hapa shuleni watatu waligundulika kuwa na ujauzito, na wote hawa hawapo shuleni tumejaribu kuwafuatilia kujua wakowapi hadisasa haijulikani, na hata baada ya Waraka wa Elimu uliotolewa wa kuwarejesha kuendelea na masomo hawajawahi kurejea hata wazazi wao kufika Shuleni hapa kutoa taarifa kuhusu watoto wao hadi leo”.
Adhima yangu ya kukutana na kufanya mahojiano ya ana kwa ana na wasichana ambao walibeba ujauzito, wakiwa bado wanafunzi na kukatiza masomo haikufanikiwa kuwakuta kwenye maeneo ya Shule hizi ambazo zilionekana zina wasichana wa aina hiyo.
NINI KIFANYIKE?
Mkuu wa Shule ya Wasichana Kilakala anaihasa jamii kujitokeza kwenye Shule ambazo watoto wao walikuwa wakisoma, kutoa taarifa za watoto wao ikiwa wanahitaji kuendelea na masomo hata kama ni nje ya shule hiyo kwa kupewa uhamisho ofisi zipo wazi. Kama ambavyo wazazi wengine walivyo fanya ilimradi tu mtoto asipoteze ndoto zake alizo kuwa nazo.
Mwl. Delphine Gervas kutoka katika Shule ya Sekondari Kayenzi anasema, Wadau wa elimu na jamii kwa ujumla waendelee kutafuta mbinu za kuongea na wasichana walio wahi kubeba ujauzito wakiwa bado shuleni. Waweze kuelewa na kuona umuhimu wa elimu katika maisha yao ya sasa na baadae kwani elimu itawakomboa siotu kujua kusoka na kuandika, bali hata kupambanua mambo yanayo faa na yasio faa kutenda katika jamii.
JICHO LA MWANDISHI WA MAKALA HII:
Nizaidi ya miezi kumi sasa, tangu Waraka wa Elimu utolewe na kuanza utekelezaji wake kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia, ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa Waraka huu unaonesha bado mwitikio wake kwa walengwa ambao ni wanafunzi wakike walio katiza masomo kwa kubeba ujauzito sio mzuri.
Serikali yaweza kuweka mkakati maalumu wa kuwabaini wanafunzi hao walipo, na namna ya kuwafikia ili wapewe elimu ya unasihi wakina utakao wafanya kueliwa na kureje masomoni.
Na, John Kabambala.