Sauti za wananchi na wadau wa maendeleo husikika wakisema “miaka kumi na nane (18) nakuendelea ndio umri sahihi wa kuoa nakuolewa nchini Tanzania na si chini ya hapo” huku Sheria ya ndoa ikiruhusu wasichana wenye miaka 14 kuolewa kwa ruhusa maalum ya wazazi, na wasichana wenye umri kuanzia miaka 15 kuolewa iwapo umbile lao linaonekana kubwa.
Karibu uambatane nami iyajuwe mengi zaidi katika Makala hii inayo mlika athari za ndoa za utotoni kielimu, tukizichungulia nyaraka na kufanya mahojiano kutoka katika makundi tofauti tofauti kwenye jamii wanavyo zungumzia kwa mukutadha mpana wa ndoa za utotoni, hususani wananchi na wadau wamaendeleo ya mtoto.
TATIZO LA NDOA ZA UTOTONI
Tangu mwaka 1971 Tanzania imeendelea kukumbatia baadhi ya vifungu vya Sheria ya ndoa ambavyo kwa sasa vinaonekana wazi wazi kuwa vinamadhara ya kiafya, kielimu na kiuchumi kwa watoto wanao ozeshwa katika umri mdogo, karne hii ya 21 uwezo wa kung’amua, kudadisi na kuhoji jambo furani linalo onekana kuwa na utata umeongezeka kwa kiasi kikubwa katika jamii.
Upo uhusiano mkubwa kati ya umri wa kuolewa na mafanikio
ya kielimu, na viwango duni vya elimu ya msingi na ujuzi wa kusoma na kuandika, Benki ya Dunia iligundua kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya ndoa za utotoni na elimu ya wasichana.
Karibu wasichana wote (99%) walio olewa katika umri wa miaka 15-19 nchini Tanzania hawaendelei na masomo shuleni, ni 1% tu ndio wanaendelea, kwa wanawake wa rika lilelile ambao hawajaolewa, karibu nusu yao (45%) wanaendelea na masomo shuleni.
SABABU ZINAZO SABABISHA TATIZO HILI
Ukinzano wa vifungu vya Sheria, Katiba, mikataba na matamko ya umri wa mtoto, Umasiki wa kipato katika familia, Jamii kuendeleza tabia za unyago usio salama kwa watoto, Ukosefu wa elimu kwa wazazi na wasichana wenyewe juu ya masuala ya Afya ya Uzazi, Ukosefu wa elimu ya ujinsia, Madhara ya mapema na ya muda mrefu yanayo weza kumpata mtoto wakike atakae ingia kwenye ndoa katika umri mdogo hivi vyote nimiongoni kati ya visababishi vya ndoa za utotoni.
Kupunguza ndoa za utotoni na kuwa elimisha wasichana kunaweza kuleta matokeo chanya na makubwa kwa maisha yao ya baadaye, kuendelea na masomo yao shuleni kwa muda mrefu na kunasaidia kufikia malengo yao maishani pasipo vikwazo.
Wasichana ambao huolewa katika umri mkubwa wanakuwa na elimu bora, wanapata kazi nzuri, wanakuwa na watoto
wachache, watoto wao wanakuwa na afya bora, na wana ushawishi mkubwa katika maamuzi muhimu kwenye ngazi ya kaya, jamii na hata mchango mkubwa katika taifa lao.
Katika Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro kata ya Changalawe nimezungumza na Felistas Kalomo ambae ni mkurugenzi wa shirika la Childhood Development Organization (CDO), amesema ndoa za utotoni zinazorotesha maendeleo ya watoto hususani wakike, mtoto wa kike anapoozeshwa katika umri mdogo athari mojawapo ni msongo wa mawazo inamaana kiwanda cha kuzalisha mawazo chanya katika maisha yake hakitazalisha tena, bali mawazo ya kujiona mnyonge,kujikataa mwenyewe mwisho wake anyone hana umihimu wa kuendelea kuishi duniani kwa sababu jamii imesha onyesha si mtu mwenye umuhimu kama ilivyo kuwa mwanzo.
Bi, Kalomo anasema milango mitano yote ya fahamu haita fanya kazi ipasavyo, katika kupambanua jambo, hatakua na furaha ya tendo la ndoa maana akili yake haita kuwa na utambuzi wa masuala yanayo husu ndoa, malengo yake yalikuwa kujakuwa Daktari, muhandisi,mwalimu au mgunduzi na sasa yamekatishwa na hana matumaini ya kuyatimiza tena, hali hii humuongezea mfadhaiko wakati wote.
Kwa mujibu wa taarifa ilio chapishwa na Benki ya Dunia nchini Tanzania inaonesha mwaka 2019, Kila mwaka ndoa za utotoni zinaongeza hatari ya wasichana kutomaliza elimu ya sekondari kwa asilimia pointi 6%, Kila mwaka wa elimu ya sekondari unapunguza hatari ya kuolewa utotoni wasichana kwa asilimia pointi 17%.
Aidha taarifa hiyo ya Benk ya Dunia inafafanua kwamba kila mwaka wa elimu ya sekondari unapunguza hatari ya msichana kuzaa mtoto akiwa bado mdogo kwa asilimia pointi 9% na kuhitimu elimu ya sekondari kwa wanawake wote kunawaongezea uwezo wa kufanya maamuzi kwa 22% kwenye familia zao.
Kwa upande wake Aplonia Milambo kutoka Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro anasema Mtoto wakike anapo kosa elimu maisha yake yote yatakuwa ya kuhangaika, na matokeo yake anapo ozeshwa na majukumu ya kutunza familia yakimzidi maamuzi yao nikujinyonga au kutupa mtoto, maana anaingia kwenye ndoa akili yake bado ikiwa inatamani kukaa na watoto wenzeke na kucheza michezo ya utotoni.
“Serikali inasema mtu mwenye umri wa miaka kumi na nane (18) nakuendelea ndio anaruhusiwa kushiriki shughuli zote za maendele nchini, ikiwa ni pamoja na kuwa na maamuzi yake mwenyewe, kuruhusiwa kujitegemea, kulipa michango na kodi ya Serikali, wakati huo inaruhusu ndoa kuanzia miaka kumi na nne (14) kwa ruhusa ya wazazi, na umri wa mika kumi na natano (15) iwapo umbile lake linaonekana kubwa, kwa lugha nyingine Serikali haipingi ndoa za utotoni bali inaruhusu na mwenye mamlaka kwa mtoto imewaachia wazi “Aplonia Milambo amesema.
Ripoti ya utafiti ulio fanywa na Shirika la Twaweza Nisisi inasema, wanawake walioolewa utotoni wana uwezekano mdogo wa
kupata kazi ya kitaalam au inayohitaji ujuzi kwa maana hawana elimu ya kazi hiyo, wana uwezekano mkubwa wa kufanya kazi za kilimo, kwa wanawake ambao wameolewa utotoni wanawake sita kati ya kumi (60%) hufanya kazi za kilimo, ikilinganishwa na wanawake wanne kati ya kumi (39%) ambao wameolewa wakiwa na umri wa miaka ishirini au zaidi.
Wanawake walioolewa katika umri mkubwa (14%) wana uwezekano mkubwa wa kufanya kazi za kitaalam, kitaaluma au kazi zinazohitaji ujuzi kuliko wenzao walioolewa utotoni (3%), huo ndio utauti wa makundi hayo mawili ya wanawake katika maisha, alie olewa na ndoa ya utotoni na walio olewa katika umri mkubwa.
UTATUZI WA TATIZO HILI:
Felistas Kalomo anashauri vifungu vya Sheria vinavyo kinzana vipitie upya na kufanyiwa marekebisho dhidi ya haki na usawa kwa watoto wakike.
Aplonia Milambo yeye anasema viongozi bora wakesho huandaliwa sasa, Serikali inabidi ichukue hatua leo nasio kesho, ili kupata viongozi watakao weza kujenga hoja na kuzisimamia nilaziama familia, jamii na taifa liwaandae leo, kama Serikali haioneshi umoja katika miongozo yake kuhusu umri wa mtoto suluhisho lake kizazi hadi kizazi halitapatikana.
Na,John Kabambala.