Ndoa za utotoni ni ndoa ambayo mmoja au wote wawili wana umri wa chini ya miaka 18, jambo hali linatajwa kua ni ukiukwaji wa haki za binadamu za watoto. Licha ya kupigwa marufuku na sheria, matamko na mikataba ya kimataifa, inaendelea kuwaibia mamilioni ya watoto chini ya umri wa miaka 18, hasa wasichana, duniani kote utoto wao.
Ndoa za utotoni zinawanyima wasichana haki yao ya kufanya maamuzi muhimu kuhusu afya na ustawi wao, Inawalazimisha kutoka nje ya elimu na kuingia katika maisha ya matarajio duni, na hatari kubwa ya vurugu, unyanyasaji, na vifo vya mapema. Ndoa za utotoni huendeleza umaskini, ukosefu wa usawa na ukosefu wa usalama na ndivyo kikwazo kwa maendeleo ya kimataifa.
TATIZO LA NDOA ZA UTOTONI
Kuelewa na kutatua changamoto zinazoendeleza mila hii mbaya nchini Tanzania ni muhimu, hasa kwa vile maamuzi ya wazazi kuwaozesha watoto wao wa kike katika umri mdogo mara nyingi huchochewa na nia ya kufanya yaliyo bora kwao, hasa katika jamii ambazo ni chache. fursa za elimu au kiuchumi.
Mikataba ya kikanda na kimataifa inayokataza ndoa za utotoni ambazo Tanzania imetia saini kifungu cha 5 cha Itifaki ya Haki za Wanawake Barani Afrika kwa Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na Watu (inayojulikana kama ‘Itifaki ya Maputo’) inakataza na kulaani aina zote za mila zenye madhara ambazo zinaathiri vibaya haki za binadamu za wanawake.
Mkataba wa Afrika wa Haki na Ustawi wa Mtoto unaamuru ulinzi wa mtoto wa kike dhidi ya mila mbaya kama vile ndoa za utotoni, ndoa za utotoni ni ukiukaji wa Kifungu cha 16(2) cha Tamko la kimataifa la haki za kibinadamu, ambacho kinasema kwamba “Ndoa itafungwa kwa uhuru na ridhaa kamili ya wale wanaotaka kuoana.”
CHANZO CHA NDOA ZA UTOTO NCHINI TANZANIA:
Mwalimu Rajabu Chiwinga ni mkaazi wa kata ya Kisaki Wilaya ya Morogoro Vijijini Mkoani Morogoro, anasema kwa kiwango kikubwa zinasababishwa na umasikini wa kifedha katika familia hali inayo chochea baadhi ya familia/wazazi kuona suluhisho la umasikini huo nikuozesha watoto wadogo, jambo ambalo siokweli.
Kwa mkutadha wa kiuchumi familia zinazo ozesha watoto wadogo, hawana elimu muhimu ya kiuchumi, elimu ya afya ya uzazi, elimu ya ujinsia “huku nilipo kunawa watoto ambao walifahuru kwendelea na elimu ya Sekondari ila wazazi wao hawakuwapeleka shule, nikaaanza kufuatili ili watoto hao waende kujiunga na elimu ya Sekondari, kwa hiyo ukiona taarifa kama hiyo kama hakuna wafuatiliaji ndio mwanzo wa wazazi kuwaozesha watoto wao katika umri mdogo” Alisema Rajabu Chiwinga.
Kifungu cha 16 cha Mkataba wa Kutokomeza Aina Zote za Ubaguzi dhidi ya Wanawake (CEDAW) kinasema kwamba wanawake wanapaswa kuwa na haki sawa na wanaume ya “kuchagua kwa hiari mwenzi wa ndoa na kuolewa tu kwa ridhaa yao huru na kamili”, na kwamba. “
Kwa kutia saini Mkataba wa Haki za Mtoto (CRC), Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejitolea kuchukua “hatua zote zinazofaa na kwa nia ya kukomesha mila zinazoathiri afya ya watoto,” ambayo inajumuisha mazoea na ndoa za utotoni.
Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa yanatoa wito wa Usawa wa Jinsia, huku Lengo namba 5.3 likitoa wito mahususi kukomeshwa kwa mila potofu ifikapo mwaka 2030, zikiwemo ndoa za utotoni na za kulazimishwa.
Pili Mjuni kutoka Morogoro Vijijini anaesema ndoa za utotoni si kwamba zina madhara kwa mtoto mwenyewe tu, bali hata kwa family, jamii, taifa na viongozi wanao simamia mamlaka zenye kutoa maamuzi juu ya vifungu vinavyo ruhusu ndoa za umri wa miaka kumi na nne (14) na miaka kumi na tano (15) hata kama ni kwa ruhusa maalumu kutoka kwa wazazi.
“Wasichana hawa walitaka kuwa wauguzi, wafanya biashara/wajasiriamali, washonaji nguo, wanaojishughulisha na kilimo cha kisasa, walimu na wahasibu, ndoa na majukumu ya kulea watoto yanavuruga mipango yao ya kutimiza malengo hayo” Alisema Pili Mjuni kutoka Morogoro Vijijini.
Serikali zinatakiwa ziwe na sheria wazi na thabiti zinazotamka miaka 18 kama ni umri wa chini wa kuingia kwenye ndoa. Ulinzi wa kutosha unatakiwa uwepo ili kuhakikisha ruhusa ya wazazi na vizuizi vingine havitumiwi ili kulazimisha wasichana waolewe kwa nguvu.
MATOKEO YA MAISHA YA KIJAMII
Salome Sengo Yeye ni mchumi na mkurugenzi wa taasisi yaLadies Talk Tanzania nilitaka kufahamu kutoka kwake ni athari gani za ndoa za utotoni kiuchumi? Anasema huongeza umaskini na inaweza kusababisha mzunguko wa umaskini baina ya vizazi na vizazi, huongeza ukatili wa majumbani na Uwezekano mkubwa zaidi wa ukatili wakijinsia, ndoa za utotoni hupunguza fursa za kiuchumi kwa wasichana.
Bi, Sengo anafanua kwamba, ndoa katika umri mdogo ni uporaji wa haki za binadamu, Ukiukwaji dhidi ya haki za watoto na wanawake, hukatiza uhuru na wasichana kushindwa kutoa maoni na mahitaji yao kwa uwazi kwa wazazi, ndugu, viongozi au kweny jamii inayo wazunguka, matokeo yake wanachukua jukumu la kujiua chanzo chake kikiwa ni ndoa na msongo wa mawazo.
Kwa mujibu wa Bank ya Dunia Nchini Tanzania, “Duniani, ndoa za utotoni hupunguza kipato cha mwanamke katika maisha yake kwa asilimia 9%, hasa kwa sababu wanaoolewa mapema huacha shule mapema.” inaonesha jumla ya thamani ya mapato yaliyopotea kutokana na ndoa za utotoni mwaka 2015 yalikuwa dola za Kimarekani milioni $637M.
Faida za kiuchumi za kukomesha ndoa za utotoni (nchini Tanzania) ni kubwa sana katika nyanja za ustawi wa watu, wakiwa wanaongezeko kwa idadi ndogo, ifikapo mwaka 2030 inaweza kufikia dola bilioni $5bn za Kimarekani.
NINI KIFANYIKE?
Pili Mjuni anasema kuna umuhimu mkubwa nchi kuwa na umri wa chini wa kuolewa/kuoa kisheria, ili kuwalinda watoto wakike na wakiume wasiingie kwenye ndoa wakiwa katika umri mdogo na siyo tayari kimaumbile, kiakili na kihisia.
Jambo hili nimuhimu lijadiliwe ndani ya Bunge kwa kupewa uzito na umuhimu wake, kwa sababau wabunge wanadhamana ya kuamua na kupitisha jambo katika masirahi ya wananchi.
Rajabu Chiwinga anasema jamii itapaswa kumbua kuwa elimu nimuhimu siotu kwa maendeleo ya taifa bali hata kwa mtoto wa kike na wakiume, hivyo ni bora kuachana na taratibu za kizamani kuozesha watoto wadogo kwani niukiukwaji wa haki za mtoto.
Uchumi hauwezi kuchengwa kwa mtu ambae hana maarifa katika ngazi ya mtu mmoja mmoja, familia, jamii, nchi na hata duniani kote, nan chi zilizo endelea kiuchumi zinawekeza kwenye elimu kwa wote kuanzia watoto hadi watu wazima, hivyo basi waowaji na waozeshaji watashindwa kuoa au kuozesha endapo vifungu vya Sharia vitazungumza lugha moja Bi, Sengo amesema.
Na, John Kabambala.