Kituo cha kulelea watoto mchana cha Valentine Day care kilichopo Mtaa wa Reli Kata ya Mazimbu Mjini Morogoro kimedizi kufanya vizuri katika kutoa malezi, makuzi na maendeleo ya awali ya Mtoto ambapo kwa Mwaka 2022 kimefanikiwa kutoa watoto watano wanaotarajiwa kujiunga na Darasa la kwanza Mwaka 2023 ikiwa ni mafanikio makubwa tangu kianzishwe Mwaka 2019.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Kituo hicho, akizungumza katika mahafali ya Tatu yaliyofanyika mwanzoni mwa Mwezi Disemba, Margreth Valentine Chuwa alisema wanajivunia mafanikio hayo makubwa waliyofikia na kuwaomba wazazi na walezi waliopo ndani nan je ya Kata ya Mazimbu wanawapeleka watoto kwa Mwaka wa malezi na msomo 2023.
Margreth alisema “kituo chetu kimeanzishwa Mwaka 2019 hadi sasahivi tuna Mahafali ya Tatu, tumetoa wanafunzi watano kwenda Darasa la kwanza 2023, Mwaka 2020 katika Mahafali ya kwanza tulitoa wanafunzi wawili na Mwaka wa jana 2021 tulitoa wanafunzi watatu, kwa hivyo utaona haya ni mafanikio makubwa kwetu katika Historia ya Valentine Day Care, Ada yetu ni Laki Tano na Elfu sabini kwa Mwaka kwa watoto wanaofika asubuhi na kuondoka saa Kumi jioni na kwa wale wanaofika Asubuhi na kuondoka saa Sita mchana Ada yao ni Shilingi Laki tatu na Elfu sabinitu. tunashukuru sana kituo chetu kinazidi kupata Baraka, watoto tunawalea vizuri, wanapata Afya nzuri hata wazazi wanafurahia malezi ya watoto wao”.
Hadija Yusuph mzazi wa Samir Hamis Mtoto aliyehitimu Elimu ya Kindagaten alitoa shukrani zake kwa niaba ya wazazi wengine, akipongeza kituo cha Valentine Day care kwa kutoa malezi bora ya watoto. “tumekuwepo hapa Valentine Day care kuwapongeza watoto wetu waliomaliza Elimu ya Chekecheka kujiandaa na Elimu ya Msingi, Kituo hiki ni kizuri hivyo nawashauri wazazi wenzangu walioko majumbani kuwaleta watoto wao, ni Kituo kinachowalea watoto vizuri kinidhamu, kielimu, kimaarifa zaidi na wako vizuri katika malezi ya watoto” alisema Mzazi Hadija Yusuph.
Stella Ernest Mapunda Mwalimu Mlezi wa Valentine Day care Centre anasema Elimu na malezi wanayotoa kwa watoto ni bora na kwamba changamoto anazozipata katika kazi yake hazikwamishi watoto kupata malezi mazuri.
Madam Stella alisema “Katika kituo chetu tunatoa malezi ya watoto wa kwanzia Mwaka mmoja hadi Miaka mitano, mbali na malezi pia tunatoa Elimu ya awali, wapo watoto wadogo zaidi ambao wanahitaji kuangaliwa kwa makini sana, mimi natumia uwezo na uzoefu wangu natengeneza urafiki nao na hatimaye wananizoea na kuwa wananielewa, tunawalea vizuri kwakweli na wote tunazingatia ratiba yao katika muda wa masomo, muda wa kucheza, muda wa kula na muda wa kulala.
Chakula ni kizuri wanakula matunda, Wali na Ugali lakini watoto wengi wanapendelea kula Wali na matunda, kama ikitokea akawepo anaebagua vyakula tunampa chakula tofauti na hiko, kwa mfano Mtoto hapendi Wali tunampa Ugali na kama hapendi Ugali tunampa Wali. Nichukue nafasi hii kuwakaribisha tena wazazi katika Kituo chetu cha Valentine Day care wawalete watoto wapate malezi na Elimu ya awali.”
Margreth Valentine Chuwa alitoa rai kwa wazazi na walezi juu ya changamoto ya kutolipa Ada kwa wakati, akiwataka kujitahidi kulipa Ada ili kutokwamisha watoto kupata malezi bora. Margreth alisema “Changamoto kubwa iko kwa wazazi wengine huwa wanafikiri tuna msaada tunaopata ili kulea watoto kumbe hakuna, sisi tunategemea zaidi Ada zao ili kuendesha Kituo, kwakweli inasikitisha lakini mimi niwaombe wazazi wajitahidi kulipa Ada za watoto kwa wakati ili haya manufaa Yazidi kuwepo na wao waendelee kufurahia”
Na, Hamad Rashid