duniani,madhara ya mabadiliko ya tabianchi tayari yanadhihirika wazi katika
maeneo mbalimbali kamavile Njaa, Ukame
na Mafuriko yanayoharibu maisha ya mamilioni
ya watu na kuwaweka katika hatari zaidi ya kukabiliwa na njaa, kukosa makazi, matatizo
ya kiafya nahata kupelekea vifo vya watoto na wazee wasio weza kujiokoa wenyewe.
“Usiku ule kuanzia majira ya saa sita
sitausahau, ulikuwa niusiku wa kuamkia January 13, 2023, mvua kubwa ilinyesha
isiokuwa na miungurumo,radi wala upepo, kwa takribani masaa 7 hivi, ndio muda
mvua ile iliutumia kunyesha, Manispaa ya Morogoro ilionekana kwa mwanga wa taa
za umeme tu, nasio taa za magari barabarani, bilasha hata magari hayakuweza
kuendelea na safari zake za usiku kama ilivyo kawaida siku zingine kusafiri
usiku.
Haiukuwa rahisi kudhani kwamba maji ya mvua ile
yangejaa ndani ya nyumba kiwango cha kimo cha futi tano vyumbani hata sebuleni,
kwa sababu nikiwa kitandani nilijua tu
ni mvua ya kawaida” Mwanabibi Sefuchuto
miongoni mwa wa athirika wa mafuko Manispaa ya Morogoro.
“Ninapo
yaona mabaki ya madufutari na vitabu vyangu hivi najisikia uchungu, kwani
mafuriko yaliingia chumbani kwetu usiku wa manane hata mama mdogo alisinzia
fofo wakati bibi anagonga mlango kutuita tufungue, mimi ndio nilie anza kuamka,
niliposhusha miguu chini ya kitanda nakanyaga maji kimo cha kufikia kiunoni
kwangu.
Ndipo lipo anza kupiga kelele na mama mdogo akaamka
nakufungua mlango wakati huo nikaona vitu vikaanza kuelea juu ya maji likiwemo
begi langu la madafutari nguo za shule pamoja na viatu, nilikosa masomo kwa
kipindi cha siku 10 hivi, lakini pia nilishindwa kuonana na marafiki zangu
shuleni na kucheza pamoja, lakini sasa nimesharejea shuleni kuendelea na masomo ” huyo ni Samira
Msemwa mwanafunzi anae soma darasa la sita shule ya msingi Azimio.
LA MAFURIKO:
Tatizo huaribu miundo mbinu, makazi ya binadamu kamavile majengo ya
nyumba, kusababisha njaa, magojwa nahata vifo kwa watoto wadogo, wazee na
wanawake wasio weza kujiokoa wenyewe.
Mvua hiyo ilinyesha maeneo mbalimbali katika
Manispaa ya Morogoro ambapo mikondo ya maji ilitiririsha kiasi kikubwa cha maji
yaliyosababisha mafuriko kwenye mitaa ya Azimio kasikazini katika Kata ya Kihonda pembezoni mwa barabara
kuu itokayo Dodoma kuelekea Dar es salaam.
Mafuriko hayo yalizingira makazi ya wananchi
kwenye eneo hilo ambapo kwa tathimini ya makazi yalio halibiwa nizaidi ya kaya 200 zilizingirwa na mafuriko
hayo kati ya kaya 2192 kwa mujibu wa ofisi ya mwenyekiti wa mtaa wa Azimio, na kufanya kaya hizo kuhitaji msaada wa makazi, chakula na misaada mingine
ya kibinaadamu.
KIKUBWA CHA MAFURIKO HAYO:
Mwanabibi Sefuchuto ni mkaazi wa Azimio Kihonda baada ya kufanya mahojiano nae
amesema, katika eneo hilo anazaidi ya miaka 20 tangu ahamie na kuishi kwenye
makaazi yao hayo, na kila mwaka mvua hunyesha pasipo madhara kama yaliotokea
mwaka huu.
“Chanzo kikubwa cha mafuriko hayo anasema ni
baada ya ujenzi wa mradi wa reli ya mwendo kasi ulivyo anza, mifereji iliokuwa
ikitiririsha maji kwa miaka yote hiyo na madaraja, wameibadilisha mwelekeo wake
na mingine imezibwa kabisa, mafuriko yalio bomoa makazi yangu hapa mradi wa
mwendo kasi wameweka daraja amabalo lina matundu sita (6) yakutolea maji, na
matundu hayo yameelekezwa kwenye makaazi ya watu pasipo kuyatengenezea mtalo
mkubwa unao endana na ukubwa wa daraja hilo.
Hivyo basi baada ya mvua kubwa kunyesha maji
yalijaa kwenye mfereji wa zamani ambao hata hawakuujengea tangu wakandarasi walipo
fanya mabadiliko ya ujenzi wa barabara ya Reli na kuweka madaraja mapya”
amesema Mwanabibi Sefuchuto.
YALIO JITOKEZA:
Watoto hawakwenda shule kwa kipindi cha karibu siku kumi (10) kwa sababu Vyakula
vilisombwa na maji na yamesababisha ukosefu wa chakula cha kutosha, na hata
watoto wasinge kwenda shule bila uhakika wa kula ukizingatia shuleni hakuna program
ya chakula, vyombo vya ndani, magodoro, kuku walisombwa na maji, madafutari,
vitabu, sale viatu vya shule vya watoto, mabegi, na nguo zetu zingine zikafukiwa
kwa tope la maji hayo, kama unavyoona sasa ndio ninazifua.
NJIA IPI
WALIITUMIA KUJIOKOA:
Unaona kwenye kijumba hiki ambacho kama cha gorofa ndipo tulipo ponea
baada ya maji kujaa ndani kwenye vyumba vyote, tuliwachukua watoto tukawapandisha
hapa juu na sisi wenyewe tukapanda hapa kusubiria msaada utakao tufikia pengine
asubuhi, maana tulikaa hapa kuanzia saa tisa za usiku hadi saa moja asubuhi sisi wakubwa tukashuka maji yalipo
anza kupungua lakini vitu vingi vilikuwa visha sombwa na maji.
Mwenyekiti wa mtaa wa Azimio Ndg, Michael
Bendera ameeleza chanzo cha mafuriko hayo kua ni “mabadiliko ya eneo hili kwenye mtaa wangu, na
mabadiliko haya yamesababishwa na ujenzi wa reli ya mwendo kasi, zamani maji yalikuwa yanapita lakini sio kama ya
awamu hii, Mitalo mingi imeelekezwa kupitisha maji kwenye eneo moja, madhara
makubwa nikuharibika kwa makaazi ya watu na vyakula kusombwa na maji huku familia
kubaki bila dira na watoto ndio walikuwa wahanga wakubwa wa njaa na elimu kwa
takribani siku 10”.
Aidha Michael Bendera amesama
kabla ya mvua hii kubwa haijanyesha na
ksababisha mafuriko alimfuata afisa mazingira wa Manispaa ya Morogoro
kumuonyesha na kumueleza namna ya kuchimba na kuujengea mtalo maji ili hata
mvua itakapo nyesha pasiwe na madhara kwa makazi ya wananchi, lakini hakuna
hatua yeyote iliochukuliwa kupitia ofisi ya mazingira zaidi ya miezi sita sasa.
“Hata baada ya mafuriko afisa mazingira alikuja nikaenda nae hadi kwenye
eneo hilo la mtalo uliosababisha madhara kwenye makazi ya wananchi, ilikuona
tena uwezekano wa kuuongeza kina na kuujengea na afisa mazingira mwenyewe alipokanyaga kwenye tope lililotuama
viatu vilibaki humo, richa ya kujionea
hayo yote hakuna hatua yeyote mpaka sasa nina uhakika endapo mvua kubwa
itanyesha tena kama sio kufa watu basi uharibifu mwingine utatokea”Alisema Michael Bendera.
Aalie kuwa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro
Mjini Albert Msando alisema “Chanzo
cha mafuriko hayo sio ujenzi wa Reli ya mwendo kasi bali ni ujenzi holela
usiofuata mipango miji”.
Mwanabibi Sefuchuto matarajio
yake na kilio chake kipo kwa mamlaka husika za serikali kuona ni njia gani
itatumika kuhakikisha mtalo huo unatafutiwa ufumbuzi kwa kujengewa kuelekea mto
ngerengere.
“Ofisi ya mazingira itekeleze ahadi zake juu ya
kuongeza kina cha mtalo huo na kuujengea mwanzo wa daraja la mwendo kasi hadi
mto ngerengere kama ambavyo wananchi wamtaa wa Azimio wamekubariana, na kama
serikali haitaki kuchimba na kujengea mtalo huo wananchi wamsha pitisha
kuchanga Tshs, 10,000/= kwaajili ya
kununu mafuta ya greda litakalo chimba mtalo huo”, alisema Michael Bendera.
Kauli ya serikali kupitia kwa alie kuwa Mkuu wa
Wilaya ya Morogoro Mjini Albert Msando, “ni kwamba wananchi wamejenga kwenye vyanzo vya
maji, hivyo wanapaswa kuhama”.
Na, John Kabambala-Morogoro.